NA MWANDISHI WETU
MAFIA Joaquin Guzman, aliwahi kutoroka katika Gereza mara mbili kwa nyakati tofauti, tena likiwa Gereza lenye ulinzi mkali, lakini baadae alikamatwa tena na alihukumiwa kifungo cha maisha gerezani.
Ni baada ya kupatikana na hatia katika makosa 10 yakiwemo ya kusambaza dawa za kulevya, utakatishaji fedha, na kujihusisha na uuzaji wa dawa ya kulevya.
Katika chumba kidogo chenye umbo la L,mwishoni mwa korido katika Gereza la Altiplano Mexico, kulitokea moja ya utoro uliofanywa na mahabusu aliyekuwa katika jela hiyo ambayo ina shimo dogo sakafuni katika chumba kidogo cha bafuni.
Kwa kupitia shimo hilo dogo, ndipo Mafia huyo aliyekuwa akijihusisha na madawa ya Kulevya, Joaquin Guzman, au maarufu kama El Chapo, alipotorokea nje ya Gereza hilo, lenye ulinzi mkali siku ya jumamosi usiku baada ya kuwekwa hapo kwa miezi sita tu.
Shimo hilo linalotokezea upande mwingine wa handaki la kisasa maili kadhaa, mbali na kutoroka, cha ajabu ni kwamba kwa mara nyingine tena tukio hilo likageuzwa na kuonekana ni suala lililotokana na watu fulani kupewa rushwa na njama miongoni mwa uongozi wa Gereza hilo.
Serikali iliwaruhusu waandishi wa habari kutembelea jela hiyo alimokuwa amewekwa Guzman, Shimo alipotorokea lilikuwa na vipimo vya takribani Sentimeta 50 (futi 1.5).
Kila upande lilionekana kuwa na sakafu katika eneo la bafu la kuogea na lilikuwa ni dogo lenye inchi chache tu, lilikuwa kidogo na giza ambalo lilikuwa ni vigumu kuona na kulikuwa hakuna dalili zozote kuwapo kwa ngazi ambayo aliitumia Guzman kushuka chini ya handaki hilo.
Katika jela hiyo pia kulikuwa na sinki la kuogea pamoja na choo, kinyesi, saruji na kipande cha mbao imara ambacho kinaonekana kiliwahi kuwa ni dawati, dirisha lilikuwa limezuiwa kwa juu katika ukuta wa nje ambapo linaruhusu hewa kidogo kuingia na kutoa muonekano wa nje kupitia mwanya huo ambao ulikuwa umezuiliwa na nyaya za usalama, ikilinganishwa na kiasi cha rangi ya bluu bahari.
Lakini pia mahali ambapo kulikuwa na shimo hilo kulikuwa kunalindwa na kamera ya ufuatiliaji ambayo ilikuwa imefungwa kimo cha kuanzia kifuani ili kutoa faragha kwa wafungwa wanapokuwa wanajisaidia na kamera hiyo ilipaswa kuwa inafuatiliwa muda wote, lakini haikuwa ikifuatiliwa.
Mapema mamlaka husika iliachia picha za mwisho zilizokuwa zimerekodiwa na kamera hiyo ya kiongozi huyo wa kundi lake la, Sinaloa Cartel, kabla ya kutoroka kwake. Mkanda huo uliorekodiwa na Kamera, ulionyesha kuwa alikuwa akiingia na kukagua bafu hilo lililoko ndani ya selo yake na kuelekea katika kitanda chake na kuonekana akiwa anataka kuvua viatu lakini alirudi tena bafuni akionekana akiwa na mipango mizito, na Kamera haikuweza kupata picha yake kwa kuwa alizibwa na ukuta na baada ya hapo hakuonekana tena.
Maofisa wa juu kabisa wa usalama nchini Mexico waliitisha Mkutano wa dharura wa usalama wa ndani ya nchi baadae, Maofisa walipoulizwa kuhusu ni kivipi handaki hilo lilijengwa moja kwa moja chini ya Gereza hilo bila ya mtu yeyote kugundua, wakati matengenezo mengi ya sehemu kama hizo za chini ya ardhi kuanzia futi sita chini na kupasua sakafu ya bafu mpaka kupata handaki la kutokea upande mwingine lazima sauti ingesikika tu.
Wafungwa walikuwa wako kimya wakati kikundi kidogo cha waandishi wa habari walipokuwa wakilindwa ili kupita kwenye jengo kuu kuelekea jela namba 20 wakipita milango ya chumba namba 22 iliyokuwa imefungwa na makufuli kuelekea huko.
Kutokea katika Korido ya selo ya Jirani yake Guzman, siku zote alipokuwa katika jela hiyo ilisikika sauti ya redio katika chumba cha mahabusu ambaye alikuwa akisikiliza mpira wa miguu, sauti ya mahabusu mwingine ilisikika akitulia chini kwaajili ya Chakula chake cha jioni na kumtakia Jirani yake mlo mwema.
Sehemu nyingine katika jela hiyo, mahabusu ambao walikuwa wamenyoa nywele na kuvalishwa sare walikuwa wamenyamaza kwaajili ya chakula katika eneo la jumuiya hiyo ya kulia chakula, na lilikuwa likiendelea kufungwa baada ya kupokea chakula chao.
Lakini pia bado kuliibuka maswali juu ya asili halisi ya ujengaji wa handaki hilo na ukweli ulionekana katika Kamera za ufuatiliaji ziliposhindwa kumulika wakati akiingia hapo, ilipendekezwa kuwa kuna mtu alimpa Guzman nakala ya ramani nzima ya Gereza hilo.
Serikali ilikazia kuwa Magereza ya Altiplano, ambayo yako takribani maili 90 kutoka Mexico yametimiza viwango vya ubora wa usalama na kusema kuwa Guzman lazima atakuwa amepata msaada kutoka kwa maafisa wa jela na maofisa wengine lakini pia iliahidi kuwafanyia uchunguzi maofisa wake lakini haijaonyesha dalili yoyote ya shinikizo la msukumo kwa viongozi wakuu.
Wajumbe wa makamishna walianza kuwa makini kuangalia muda ambao umepita kati ya kutoonekana kwa Guzman katika eneo lake na muda ambao kengele ya tahadhari ilianza kutoa taarifa.
Jumatatu mwaka 2015, Waziri wa Mambo ya Ndani, Miguel Angel Osorio Chong, alisema kuwa kengele ya tahadhari ilipigwa mapema lakini vyanzo vya taarifa kutoka kwa wafungwa walisema ilichukua nusu saa Polisi kuanza kumtafuta Guzman.
Hii ndio inaweza kuwa ikawa imempa uwezo wa Mafia huyo kutorokea kupitia handaki ambalo lilikuwa limejazwa vitu vya uchafu wa matofali na taa mbovu ambazo ilionekana alizitawanya ili kupata njia.
Haikuwekwa wazi kama Guzman alitorokea kupitia handaki hilo ambalo ni la futi 5 na 6 kwa ndani, ni refu linaloweza kumwezesha kusimama au kwa vyovyote hata kutumia pikipiki ambayo huenda aliikuta ndani ya shimo hilo ambayo inaonekana huenda labda ilikuwa imewekwa kwaajili ya kuondoa uchafu na vifaa.
Lakini pia kulikuwa hakuna mwelekeo wa wapi hasa alikuwa ameelekea baada ya kupanda ngazi upande mwingine wa mwisho na kurudi ardhini na kuwa huru, hapakuwa na taarifa zozote zaidi ya kuanza kumsaka.
Waziri huyo alisema karibu Askari Polisi 10,000 wako makini zaidi katika kuvuka, kuingia na kutoka Mexico, na zaidi ya kikosi maalum cha askari 500 cha utafutaji, lakini pia machapisho yenye picha ya Guzman takribani laki moja ambayo yana muonekano wake wa wakati huo ambazo zilisambazwa katika vituo vyote vya ukaguzi njia kuu, palikuwa pia na mbwa wa kunusa, lakini pia kwenye viwanja vya ndege, Askari wa Usalama walikuwa makini.
Serikali ya Mexico ilitoa zawadi ya fedha milioni 60 ambayo ni sawa na (£2.5m) kwa taarifa itakayosaidia kuongoza kukamatwa kwake, Bosi huyo wa kundi hatari la Sinaloa Cartel kwa mujibu wa mtandao wa Forbes mwaka 2015 alikuwa ni tajiri wa 14 duniani, mwaka 2001 alifanikiwa kutoroka tena katika Gereza madhubuti la Puente Grande.