Makamu wa Rais wa Cuba awasili nchini kwa ziara ya kikazi

DAR ES SALAAM-Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba, Mhe. Salvador Valdés Mesa amewasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu kuanzia tarehe 23- 25 Januari, 2024.
Mara baada ya kuwasili nchini kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Mhe. Mesa alipokelewa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb.)

Akiwa nchini, Mhe. Mesa atakutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete na pia atatembelea taasisi ya Mwalimu Nyerere.

Mhe. Mesa pia atamtembelea Mjane wa Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Mama Maria Nyerere pamoja na kutembelea kiwanda kinachozalisha dawa za viuadudu ya Biolarvicide cha Kibaha, Pwani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news