Mauzo ya bidhaa za Tanzania nchini Uingereza, Balozi Kairuki amshukuru mwanadiaspora Petronila Mlowe

LONDON-Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Uingereza, Mheshimiwa Mbelwa Brighton Kairuki amemshukuru mwanadiaspora, Bi. Petronila Mlowe kwa utayari wake kusaidia juhudi za kuongeza mauzo ya bidhaa za Tanzania katika soko la Uingereza.

Mheshimiwa Balozi Kairuki amatoa shukurani hizo kupitia ukurasa wake wa x (Twitter).
"Ninamshukuru sana Mwanadiaspora Bi Petronila Mlowe kwa utayari wake kusaidia juhudi za kuongeza mauzo ya bidhaa za Tanzania katika soko la Uingereza.

"Kwa hakika ufahamu wake mkubwa wa taratibu za uingizaji wa bidhaa katika soko la Uingereza na EU utaifaa sana nchi yetu...

"Bi.Mlowe,mwajiriwa wa Serikali ya Uingereza ana uzoefu wa zaidi ya miaka 15 katika shughuli za udhibiti wa ubora wa bidhaa za vyakula.

"Ubalozi utaendelea kushirikiana na Diaspora katika kuhemea fursa mbalimbali nchini Uingereza na Ireland,"amefafanua Balozi Kairuki.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news