NA DIRAMAKINI
NI wazi kuwa, kuishi katika baadhi ya miji Afrika unaweza kukumbana na changamoto kubwa ya matumizi ya fedha siku hizi hasa kutokana na kuongezeka kwa mfumuko wa bei.
Picha na Addis Ababa Travel.
Kwani, gharama za kila kitu, kuanzia malazi hadi chakula inaongezeka kila siku.Bidhaa za kimsingi, kama vile chakula na huduma, zimeshuhudia kupanda kwa kasi.
Aidha,kushuka kwa thamani katika masoko ya kimataifa, pamoja na changamoto katika sekta za kilimo na nishati nchi mbalimbali kunaongeza bei za bidhaa za kila siku.
Ni vigumu sana kwa kaya nyingi zinazojaribu kupata riziki kuweza kukidhi mahitaji yao.
Wakati baadhi ya miji ya Afrika imepata ukuaji mkubwa wa kiuchumi, kukosekana kwa usawa wa kipato bado ni suala linaloendelea.
Pengo kati ya matajiri na maskini linazidi kuongezeka, na hivyo kufanya kuwa vigumu kwa sehemu kubwa ya watu kukabiliana na kupanda kwa gharama ya maisha.
Ripoti ya Numbeo, mojawapo ya majukwaa ya takwimu na utafiti duniani, imefichua gharama ya maisha katika miji mbalimbali ya Afrika.
Farihisi hutumia vigezo kama vile kodi ya nyumba, bei ya vyakula,migahawa, gharama za maisha na uwezo wa ununuzi wa ndani.
Chini ni miji 10 ya Afrika ambayo ina gharama kubwa unapotaka kuishi;
Rank | City | Cost of living index | Local purchasing power index |
---|---|---|---|
1 | Douala, Cameroon | 49.8 | 6.1 |
2 | Addis Ababa, Ethiopia | 46.8 | 8.6 |
3 | Harare, Zimbabwe | 37.9 | 21.8 |
4 | Johannesburg, South Africa | 36.7 | 87.4 |
5 | Cape Town, South Africa | 35.1 | 87.9 |
6 | Pretoria, South Africa | 34.6 | 91.9 |
7 | Casablanca, Morocco | 33.7 | 34.1 |
8 | Rabat, Morocco | 33.6 | 33.2 |
9 | Durban, South Africa | 33.4 | 62.1 |
10 | Marrakech, Morocco | 32.9 | 28.0 |