NA DIRAMAKINI
DEREVA wa kusafirisha mizigo huko Fort Worth mjini Texas nchini Marekani, Scotty Jackson ameuawa na mwanaume,Christantus Omondi aliyekuwa uchi kwa kumpiga hadi kufa.
Ni kwa kutumia kuni alizokuwa akipeleka kumuuzia mteja wake, nyaraka za mahakama zinaonesha.
Raia huyo wa Kenya mwenye umri wa miaka 27 ambaye anaishi huko Texas,sasa yuko jela na anashtakiwa kwa kosa la mauaji.
Polisi wanasema, baada ya shambulio hilo la kikatili, Omondi alirejea kwenye nyumba aliyokuwa akipangisha na kutishia mpangaji mwingine.
Imeelezwa kuwa, mwathiriwa huyo alikuwa akifanya kazi yake tu, akishusha kuni kwenye makazi huko Fort Worth.
Mwenye nyumba akatoka nje kumsaidia. Mwenye nyumba aliweza kuepuka shambulio hilo.
Anasema, mshukiwa alikuwa akitenda tukio hilo la kiatili huku akionesha jeuri kubwa.
Mmiliki wa nyumba ambaye hakutaka jina lake litajwe au uso wake uoneshwe, alizungumza na FOX 4 na kusimulia shambulio hilo la kutisha.
"Niamini kabisa kwa moyo wangu wote kwamba alikuwa anataka kutuua sisi sote," alisema.
Chrisantus Omondi (Source: Tarrant County Jail).
Maafisa waliitwa kwenye nyumba hiyo huko Fort Worth siku ya Jumamosi usiku katika hali ya baridi kali, baada ya watu wengi kuwapigia simu kuwataarifu kuhusu shambulio hilo.
Polisi walimkuta Scotty Jackson mwenye umri wa miaka 51 akiwa amekufa kwenye yadi ya mbele huku akiwa na majeraha makubwa kichwani na shingoni.
Mwanaume anayemiliki nyumba hiyo aliwaambia polisi kwamba, alikuwa amempigia simu Jackson ili kununua kuni.
Aidha,Jackson alipofika na gari iliyojaa kuni, mwanaume huyo aliyekuwa uchi ambaye baadaye alijulikana kama Christantus Omondi alimfuata na kumshambulia, kulingana na hati ya kiapo ya kukamatwa.
"Mtu huyu aliyepo uchi yuko mita tatu kutoka katika uso wangu, akiwa ameshikilia ufunguo wangu akinipigia kelele kwamba nilikuwa kwenye mali yake.
"Hataki kuniona tena. Ninapaswa kuondoka," mwenye nyumba alibainisha. "Scott kisha akajibu, "Hapana, hii ni mali yake na nyumba yake. Hebu tupakue kuni kwa sababu nje kuna baridi."
Mwenye nyumba aliwaambia polisi, ndipo Omondi alipomsukuma na kisha kumpiga Jackson na kipande cha mbao mfululizo.
Aidha, inadaiwa Omondi alimfukuza mwenye nyumba na kurudi ndani kwake.
Mwenye nyumba alimtazama Omondi akirudi kwa Jackson na kumpiga kwa kuni hadi kufa.
Katika hati za polisi, maafisa walibaini kuwa mashahidi wengine walithibitisha anuani ya mwenye nyumba,kwa kufuatilia video.
Mpangaji wa kike ndani ya nyumba jirani, baadaye aliwaambia polisi kwamba alikuwa akifua nguo wakati Omondi, ambaye alimtambua kama mpangaji wa chumba kingine akitenda kosa hilo na alikimbilia ndani ya nyumba hiyo akimfokea, nyaraka zinaonyesha.
Mwanamke huyo aliwaambia maafisa Omondi alijaribu kuingia chumbani kwake kwa nguvu huku akipiga kelele, "Nitashinda... Nitakuf...wewe."
Mwanamke huyo alielekea bafuni, na Omondi alikuwa akijaribu kuingia ndani kwa nguvu polisi walipofika, kulingana na hati ya kiapo.
Polisi walimwambia Omondi aondoke nyumbani, na alipoondoka, aliendelea kumzomea afisa, nyaraka zinaonyesha.
Omondi, ambaye bado alikuwa uchi, "hakuwa tayari kutii na kufuata sheria na alikuwa mkali," kulingana na hati ya kiapo. Polisi walitumia mamlaka yao na hatimaye Omondi akazuiliwa.
Scotty Jackson. (Picha na Familia).
Kasey DeLeon anawaza siku ambazo baba yake, Scotty Jackson, aliwaacha yeye na mabinti wake wawili.
Aliishi na baba yake huko White Settlement. Lakini Jumamosi jioni, Jackson hakurudi nyumbani. "Baba yangu hunipigia simu kila mara,'" alikumbuka.
Mara ya mwisho DeLeon alisikia, Jackson alikuwa akipeleka kuni Jumamosi jioni kwa ajili ya kuuza. "Sitaweza kumpigia baba yangu tena simu. Sitaweza kumuona. Kwa wakati huu, nina chuki nyingi na hasira nyingi.Natumai tu kwamba haki itatendeka. Hiyo ndiyo tu ninayotaka kwa baba yangu."
Majirani wanasema,Omondi alikuwa amekodisha tu nyumba kwenye mtaa huo siku chache zilizopita.
Aidha, imedaiwa kuwa, Omondi ana historia ya uhalifu, ikiwa ni pamoja na kukwepa kukamatwa.
Mwaka jana, alimshikilia mlinzi kwa mtutu wa bunduki katika Kaunti ya Tarrant. Omondi ameshtakiwa pia kwa mauaji, kushambulia vibaya afisa wa usalama na kuzuia asitekeleze majukumu yake.(NA)