NA FRESHA KINASA
MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini mkoani Mara, Prof. Sospeter Muhongo ametembelea vijiji viwili ambavyo ni (Busamba na Etaro) vya Kata ya Etaro kutoa pole na rambirambi kwa waathirika wa maafa yaliyosababishwa na mvua nyingi zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali nchini.
Hayo yamebainishwa Januari 4, 2024 kupitia taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mbunge wa jimbo hilo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo imebainisha kuwa,"Mtoto mmoja wa mwaka mmoja na nusu alifariki baada ya kuangukiwa na ukuta uliobomoka kutokana na mvua nyingi iliyonyesha kwa siku kadhaa mfululizo.
"Mbunge wa jimbo ametoa rambirarambi zake kwa familia ya mfiwa," imeeleza taarifa hiyo na kuongeza kuwa.
Aidha,taarifa hiyo imeeleza kuwa, "Familia zaidi ya kumi na tano zimebokewa nyumba na kwa sasa familia hizo zimehifadhiwa na majirani na ndugu zao.
"Mbunge wa Jimbo amewapa fedha za kujikimu maisha kwenye wakati huu mgumu.
"Mbunge wa Jimbo anaendelea kufuatilia maafa yanayosababishwa na mvua nyingi zinazoendelea kunyesha vijijini mwetu."
Picha za hapa juu ni Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo, akiwafariji waathirika wa mvua zilizosababisha maafa makubwa ndani ya Kata ya Etaro.