NA GODFREY NNKO
MTANGAZAJI wa Clouds FM,mwanamitandao maarufu na mwigizaji wa maigizo, Burton Mwambe maarufu kwa jina la Mwijaku amesema, kasri lake alilolijenga huko Kigamboni jijini Dar es Salaam limechukua muda wa miezi tisa.
“Nyumba hii ni ya kwangu na nimejenga mwenyewe na ninaomba niweke wazi aliyefanikisha niweze kununua kiwanja hiki ni Dahuu, kwa hiyo yeye labda awadang’anye watu awaambie kwa sababu yeye ndiye alikuja kuniambia jamani kuna nyumba inauzwa twende ukainunue ukabomoe (hapa).
“Akanichukua akanileta hapa Husna, nikaangalia nikamshirikisha mwenzagu baada ya kumshirikisha akapapenda, tukatafuta jirani tuhakiki, tukaenda tukauliza akasema hamna matatizo, ndiyo tukafanya process ya kuvunja.
“Kwa hiyo, labda wanaosema siyo ya kwangu waanze kumsuta Husna (mtangazaji Clouds FM),”amefafanua Mwijaku.
Ameyabainisha hayo Januari 5, 2024 huko Kigamboni jijini Dar es Salaam wakati akizindua nyumba hiyo.
“Kiwanja nilikinunua mwaka 2022. Nilivyonunua nikakiacha, kulikuwa na boma hapa nikapaacha, nikapalipia nikapaacha, ilivyofika mwaka 2023 mwezi wa pili, nikasema nibomoe nyumba ikabidi nikabomoa nyumba nikaweka fensi nikapumzika, mwezi wa tatu, nikaanza ujenzi nikamaliza mwezi wa 12.
“Toka mwezi wa tatu mpaka wa 12 nimeanza kuchimba msingi mpaka nimekamilisha, takribani miezi tisa nilijenga na nilipanga hivyo, kutokana na mwaka 2022 malengo yangu ilikuwa si kubadilisha gari, mimi kila mwaka huwa nina tabia ya kubadilisha gari.
“Ndoto yangu ilikuwa ni kujenga nyumba, na umeona sijabadilisha gari takribani miaka miwili,na siyo tabia yangu, gari huwa ninatumia ninauza nina top-up ninanunua gari nyingine, yaani nilikuwa chizi magari, lakini baadae nikakaa na mwenzangu nikasema hapana niweke kwenye nyumba,kwa hiyo nimekamilisha.Kwa hiyo, mwaka huu nina malengo mengine kabisa,”amefafanua Mwijaku.
“Kwanza kuwa, na uhakika wa ajira ninaweza kusema ndiyo imefungua vitu vingine,kwa hiyo ajira yangu ya Clouds kupata mkataba tu, ile ilinihakikishia kufanya jambo lolote hapa, kwa hiyo nyingine ni extra, sasa inategemea na jitihada zako unatafuta kazi huku ufanya unapata kazi huku unafanya.
“Kwa hiyo zile kazi extra zinaongezea, mfano mwanzo wakati ninapanunua nilikuwa na wazo fulani, lakini nimepata mkataba, riziki ninapata nje nikasema why nisijenge ghorofa, wengine wananitisha wanasema ghorofa hauwezi, ghorofa ununue nondo sijui 30 sijui 20 hapo fundi anakuambia tani…tani.
“Nikasema, sawa ngoja nijaribu kwa nini wengine waweze mimi nishindwe, kwa hiyo siwezi kusema ni kitu chepesi au kigumu, ukiwa na uhakika kwa mwezi hata shilingi laki tano ambapo hiyo laki tano umetoa labda malazi, kula, kupanga halafu laki tano imebaki unajenga nyumba,"amebainisha Mwijaku.
Katika hatua nyingine, Mwijaku amewataka wasanii nchini kuacha tabia ya kufeki maisha katika mitandao ya kijamii, kwani hali hiyo haiwasaidii.
“Mazoea ya watu maarufu ndiyo hayo ya kufeki maisha, na kama utakuwa umepita katika mitandao ya kijamii jana Ney wa Mitego ameposti kitu akasema inabidi wasanii tubadilike, tunatishana sana mtandaoni.
“Ninafikiri alikutana na msanii katika maisha yake halisi akasema, tunatishana sana katika mtandao watu hali zao ni dhofu hali, kwa hiyo mazoea ya watu tuliyokuwa tunadang’anyana mitandaoni mtu anapiga picha sehemu nzuri, hapigi picha sehemu ambayo ya kweli na halali.
“Na hili mimi nimeliona, mimi nimesafiri, nimesafiri Ulaya nimekutana na watu picha walizokuwa wanaziposti zilikuwa zinanitisha, lakini baada ya kufika Paris (Ufaransa) sehemu anayolala nikasema Subhan Allah, lakini asubuhi anavaa vizuri, anapiga picha.
“Kwa hiyo,mazoea hayo ya kutoonesha uhalisia inamaana watu wameamini na mimi hapa ninafeki, mimi nitafeki kitu kingine siwezi kufeki sehemu ya kulala, ndiyo maana hata sehemu niliyokuwa ninaishi Salasala nilikuwa ninaposti clip zangu za Mathias watu walikuwa wanasema, fagia uwanja, sijui paka rangi, nilikuwa siwezi kupaka rangi sehemu ambayo si yangu.
“Siwezi sijui kufanya nini, kutengeneza, watu walikuwa wanaongea vitu vingi, ile ni sehemu ya nyumba ya mtu nimepanga, kwa hiyo mwenyewe ndiye mwenye mamlaka nayo,afanye hivi au fanya hivyo.
“Sasa hapa leo ni kwangu, ukiniambia sehemu mbona majani yameota of-course nitamuita Mathias nitamwambia majani yameota hapo."