Mwinjilisti Temba afunguka tena,ataja kinachoangamiza viongozi wengi duniani

DAR ES SALAAM-Muhubiri na Mwinjilisti wa Kimataifa, Alphonce Temba ameendelea kusema mambo magumu ambayo yanahitaji uelewa mkubwa na utulivu wa akili na roho kuyatambua na kumfanya mtu akafunguliwa na kuelewa.
Rais mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (kushoto) akiwa Ikulu pamoja na Muhubiri na Mwinjilisti wa Kimataifa, Alphonce Temba enzi za utawala wake.(Picha na Maktaba).

Mwinjilisti Temba amebainisha hayo wakati akifafanua kuwa, Mungu anao watumishi ambao wamejinyenyekeza, wasiotaka makuu, watulivu, lakini wanafanya mambo makubwa ya kihistoria katika taifa letu.

Ifahamike kuwa, Mwinjilisti Temba ni miongoni mwa watumishi wakubwa walioinuliwa na Mungu katika karne hii ambao wamejishusha na wanafanya mambo makubwa chini kwa chini, wasiotaka umaarufu wala fedha za dhuluma na kuheshimu kile kitu ambacho Mungu ameweka ndani yao na kujiheshimu kama walivyo.

Mwinjilisti Temba ukikutana naye maisha aliyonayo na unyenyekevu alionao huwezi ukaamini japo kuwa utajifunza kwamba ni Mtumishi wa Mungu kwa sababu ni jasiri kuliko kawaida na mtu mwenye imani kali katika kuisimamia na kuamini katika Mungu wake aliyempa wito.

Hivyo katika mambo makubwa ambayo ameyafungua akizungumzia kwanza juu ya habari ya watumishi amesema, kuna aina kadha wa kadha ya watumishi wa Mungu ambao wote wametajwa katika Bibilia hususani katika kitabu cha 1Wakorintho 12, kwamba watumishi hao Mungu anawatumia katika kuponya,hekima,kufadhili,miujiza, maajabu, kuhubiri na kadhalika.

Mwinjilisti Temba anasema kuwa, siyo kila Nabii ama Mtumishi wa Mungu anaona kila kitu pasipo Mungu kumfungulia, kwamba maandiko yanasema wazi kuwa kila mtumishi Mungu amemfungulia kwa sehemu.

Hivyo, Mwinjilisti Temba anataja aina tatu ya watumishi ambapo aina ya kwanza anasema ni watumishi wa Mungu ambao wamefunguliwa macho yao ya ndani ya rohoni.

Amesema, ukikutana na mtumishi huyo ataweza kuliona jina lako, maisha ya nyumbani kwako, ataweza kuona vitu mbalimbali na kuvitaja wakiwemo ndugu zako, wagonjwa na watu waliomkosea Mungu na kukwambia wazi kwa unabii.

Mwinjilisti Temba amesema aina ya pili ni watumishi ambao wamepewa neema ya ufahamu wa mawazo ya Mungu, kwa maana ya kwamba atakavyo kuona wewe na mambo yote atakayosema na wewe, atayasema pasipo yeye kujua na kuona kwa macho na atakuwa ni Mungu moja kwa moja.

Amesema kwamba, utaona muunganiko kati yako na Mungu kwa maana ya kwamba macho yake ya kiroho yanafunguka kukuona pasipo Mungu kumjulisha wewe unaona, akili yake haitaunganishwa na unenaji wake.

"Lakini macho yake yanaona kabisa na ni Mungu anasema ndani yako na utatambua hakika, atayasema mambo yote, atasema hata una nyumba, ataweza kusema maisha yako.

"Ataweza kusema matatizo ya familia yako, kila kitu ataweza kukisema, lakini yeye hakioni kwa macho, anaweza asiuone mtaa kwa jina, anaweza asiyataje majina ya ndugu zako.

"Lakini hata kama akiyataja hayataji kwa kuyaona, anayataja kwa sababu Mungu amemtumia,"amesema Mwinjilisti Temba.
Barua ya onyo ya kifo iliyoandikwa na Mwinjilisti wa Kimataifa, Alphonce Temba kwenda kwa aliyekuwa Rais wa Zambia, Levy Mwanawasa.(Picha na Maktaba).

Vile vile amesema aina ya tatu, ni Mtumishi ambaye haijalishi anaona au haoni katika kufunguliwa kwa macho yake ya kiroho, lakini anakuwa kama Mungu.

Amesema, huyu akisema anakuwa kama Mungu kwa maana ya kwamba maandiko katika Bibilia yanaeleza kuwa ninyi ni miungu, hivyo kila mtu ana sehemu ya kuwa kama Mungu katika utendaji kazi wa ki-Mungu.

Mwinjilisti Temba anatoa mfano kwa mtumishi wa Mungu, Paulo kwamba wakati mtumishi huyo anapandwa na nyoka kwenye mkono wake.

Anasema, Bibilia inaeleza kuwa watu walioshuhudia tukio hilo wakaamua kumuita Mungu kwasababu aina ya nyoka huyo na ukali wa aina ya sumu aliyoibebeba hakuna mwanadamu angeweza kuzingwazingwa na nyoka huyo ndani ya dakika kadhaa akaendelea kuwa hai.

Hivyo anasema, ilibidi akili za wana wa Israel zimuone Mtume Paulo ni Mungu, kwamba Mungu alikuwa ndani yake na hawakumaanisha kwamba ni Mungu Muumbaji walimanisha kuwa Paulo ni hakika Mungu amemvaa na hakuna mtu aliyeona kama ni kufuru.

Amesema kwamba, katika aina hii ya tatu ya watumishi, ambayo imeenda sambamba na mfano kuhusu Mtume Paulo, hii inamuonyesha Mtume Paulo alivyo mtumishi mkuu na inaelezwa kuwa watumishi wa namna hiyo wanapatikana kwa uchache sana.

"Hawa ndio aina ya watumishi kama Benson Idahosa aliyekuwa huko Benin, Nigeria miaka ya zamani, Mtumishi wa Mungu Reinhard Bonnke, Mtumishi wa Mungu Kathryn Kuhlman, Mtumishi wa Mungu TB Joshua na kadhalika,"amesema Mwinjilisti Temba.

Amesema kwamba, watumishi hao wana nguvu kubwa sana kupita maelezo, aambapo ameeleza kuwa watumishi hao ni kama Nehemiah, Isaya, Yohana Mbatizaji, ambao walikuwepo miaka ya nyuma.

"Watumishi hawa ni bahati mbaya sana mataifa ya sasa ya Afrika hayajajua faida ya watumishi wakubwa wa Mungu ambao leo hii, wangesaidia nchi zao,"amesema.

Mwinjilisti Temba alipoulizwa kwamba yeye yupo katika eneo gani katika aina hizo tatu za watumishi, alisema yeye yupo kwenye eneo la tatu kama mtumishi Mtume Paulo.

Lakini aliweka wazi kuwa watumishi hawa baadhi yao kutokana na Bibilia wengine huwa wanapewa miba, ambayo Mungu anaweza kuamua miba hiyo kuisaidia isionekane au kuiacha miba hiyo ili nguvu ya Mungu inavyozidi kuwa kubwa juu yake iidhibiti miba hiyo.

Akifafanua maana ya miba, Mwinjilisti Temba anasema miba ni vizuizi vingine vya kibinadamu juu yao ili wasijivune, ambapo alitoa mfano kwenye Bibilia katika kitabu cha Muhubiri ambacho kinazungumzia Mfalme aliyejipanga kutaka kupigana vita, kuupiga mji mwinigine mdogo.

Alitolea mfano Tanzania Bara wapigane vita dhidi ya Tanzania Visiwani, hivyo Mfalme ama Rais aamuwe kuweka majeshi kwenda kuteketeza Burundi ama Zanzibar au Rwanda nchi ambayo ni ndogo, kwa maana hiyo inaonekana wazi mwanzo mwisho vita vya Urusi na Ukraine vitateketeza nchi ndogo.

"Bibilia inasema wakati Mfalme ameshakuwa mkaidi, ameshapanga majeshi ili kuisambaratisha nchi ile ndogo kulikuwa na Makuhani wengi.

"Wahubiri wengi kipindi hicho, lakini hakuna Muhubiri hata mmoja aliyeweza kusaidia ile vita ikatike, maandiko yanasema alipatikana mtu masikini asiye Muhubiri, aliyejazwa hekima za Mungu na maarifa, akanyanyuka, akaenda kukutana na Mfalme, akampa hekima ya Mungu Mfalme, Mfalme akaacha kupigana ile vita,"amesema.

Hivyo, Bibilia inasema mwiba wa Mfalme katika hili, alikuwa masikini na kwamba kwa kuwa alikuwa masikini hakuna mtu aliyempa heshima, lakini masikini huyu kwa ujasiri alikwenda akakutana na Mfalme akamweleza na hatimaye kusitisha vita, hivyo katika kutafakari kisa hiki utapata kuona vitu vya ajabu vilitoaka.

Anataja jambo la kwanza ni mtu masikini, Rais au Mfalme akiwa katika harakati za vita na majemedari wake wakipanga namna ya kuteketeza mji, lakini alipata nafasi ya kukutana na Mfalme, akaongea naye akaacha vita, ile nguvu ya kufanya kitendo hicho ndiyo inaitwa karama ama vipawa vya Mungu ndani yake.

Hivyo, Mwinjilisti Temba anasema unaweza ukawa na kipawa cha uongozi, kimetoka kwa Mungu na sio Muhubiri, kwamba unaweza ukawa na kipawa cha neema na sio Askofu, sio Nabii, sio Mtume na sio Mchungaji kikawa ndani yako kipekee kwa ajili ya kazi fulani.

Mwinjilisti Temba anasema kuwa, Askofu wa Maaskofu, kuwa Mchungaji Kiongozi na ukawa na umati mkubwa wa watu Tanzania au duniani hakumfanyi Mungu ashindwe kumtumia mtu masikini.

Mtu asiye na mshirika hata mmoja, mtu asiyechukua sadaka, asiyechukua mafungu ya 10 kufanya kazi kubwa zaidi ya ile unayoifanya wewe.

Anabainisha kuwa ndio maana maandiko yanasema kuwa wamepewa utumishi mambo ya Mungu kwa sehemu na kuna sehemu wamefichwa.

"Lakini kuna ile ukiwa na ujumla wake yani Mungu anatembea na wewe katika kila eneo, inaitwa Fullness Of God, kwa hiyo nataka kuzungumza kitu gani sasa hivi, maandiko yanasema katika Hosea watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa, kwa sababu wameyaacha maarifa, hata Makuhani nao wanaangamizwa,"amesema Mwinjilisti Temba.

Mwinjilisti Temba anaeleza kuwa, kizazi cha sasa kinahitaji viongozi wafalme wawe karibu na watu wa Mungu wanaoona mambo makubwa na magumu ya siku za usoni ili yawasaidie wafalme kuenenda sawa sawa.

Kwamba kama unakipaji cha uongozi au cha kuwa Rais unatakiwa kukubali Mungu huyo huyo aliyekupa kipaji hicho cha kuongoza ndio kampa mtu mwingine kipaji cha kuona mambo mengine ambayo wewe huyajui. Anasema hapo ndipo shida kubwa ya sasa ya viongozi kutambua.

"Ndugu yangu nataka ni waambie kwamba utambuzi ndiyo dawa ya kwanza ya mwanadamu, kwa mfano Mgonjwa mwenye matatizo ya Malaria, Kisukari, Presha na Magonjwa mengine mbalimbali ya hatari na yasio ya hatari anavyoanza kupata dalili za mateso hayo, kitu cha kwanza akienda kwa dakatari, daktari anachotaka kujua, pamoja na kujua historia yake, nikutambua tatizo lake.

"Na ndio maana Daktari pamoja na kusoma kwa miaka yote saba, amepewa vifaa vya kumsaidia kutambua tatizo la mgonjwa, kinachoitwa upimaji, utapimwa na vifaa na vifaa vitaonyesha tatizo lako na ndipo Dokta atakuhudumia kwa kuwa amesaidiwa kutambua tatizo lako.

"Kwamba hii siyo malaria ni UTI, hii sio UTI ni Figo, hii sio Figo ni Sukari, hii sio sukari ni Presha, utambuzi watatizo lako, lakini viongozi wengi walioko madarakani sasa asilimia kubwa wameshindwa kuelewa utambuzi wa kimungu ndiyo maana baadhi yao wanakimbilia kwa waganga wa kienyeji wawasaidie kufanya utambuzi wa siku zao za mbeleni,"amesema.

Amesesema kwamba, Mfalme au Rais akiwahusisha wanadamu kuleta utambuzi wa mambo ya baadaye ni kunajisi Taifa lake mwenyewe na matokeo yake Mungu aliyehai hubeba hasira kuu juu ya Taifa hilo na kuruhusu mapigo yalipige na kinachofanyika na viongozi wa Dini ni kuanza kupambana na kuomba rehema, kutubu kwa dhambi, kutubu kwa makosa, kuomba Mungu arehemu, Mungu abariki.

Mungu atakase na maombi mengine kadha wa kadha yanayoenenda pamoja na sadaka na sadaka za shukurani na sadaka matoleo na maombi mbele za Mungu.

Pasipo kujua wametumia mzunguko mkubwa wakufanya huduma ya kiroho kwa ajili ya Mungu kurehemu ama kuponya nchi yao.

Hivyo basi huduma ya mtu mmoja mmoja inaweza ikawa tofauti na huduma ya watumishi wenye majina makubwa, kwakuwa majina makubwa na watu kujaa na kuwa nao katika huduma yako, dhahebu lako halihusiani sana na Mungu kuwatumia watu 'special' ambao wametajwa hata katika Bibilia akiwemo Nabii Eliya.

"Maandiko yanazungumza kwa kifupi historia ya Eliya kwamba hakujulikana bali aliibuka kwenye sikeseke la matatizo ya Wana wa Israel, aliibuka kwenye sekeseke la njaa, akafika katika mlango wa Ikulu na kuanza kutabiri kwamba ndani ya masaa 24 kutakuwa na chakula kingi sana ndani ya mji ule wa Israel.

"Kutakuwa na chakula pamoja na kwamba njaa yote ambayo imekuwepo kwa muda mrefu, hakuna mtu atakayeweza kuizuia japo Mungu atakuwa amefungua milango ili chakula kijae katika mji,"amesema.

Hali hiyo ilitokea katika mazingira ambayo hakuna mtu hata mmoja ambaye angeamini kwani watu walikuwa katika hali mbaya wakila mizizi, hakukuwa na chakula mji mzima, ndipo akaibuka mtumishi wa Mungu asiyejulikana kama ni Askofu, Mchungaji wala Kuhani, hajulikani kanisa lake wala maisha yake akakataliwa na walinzi wa Mfalme kwamba hakuna mtu anayeweza kubadili hali ndani ya muda mchache na akakataliwa kumpa taarifa hizo Mfalme.

Kwamba hakuna mtu anaweza kufanya hivyo, akaambiwa ni muongo lakini cha ajabu yeye alisema neno moja kwamba mtakiona chakula kwa macho yenu, lakini akaeleza kuwa mlinzi hutakula na itakuwa ndiyo mwisho wa maisha yake.

"Basi ni kweli ndani ya masaa 24 miujiza ya Mungu ambayo ilifanyika ni mikubwa ndani ya Bibilia utaona na matokeo yake chakula kilijaa mjini, watu wakaanza kukigombania na watu waliokuwa wakikigombania ndio waliokuwa wakimkanyaga mlinzi wa Mfalme akafa barabarani.

"Ukitafakari ilikuwaje mlinzi akanyagwe, ukatafakari sauti ya mtu wa Mungu jana yake ikimwambia kwamba chakula utakiona lakini hutakula.

"Ykitafakari ni namna gani Mungu alikuwa akizungumza na mamlaka zilizokuwa duniani kwa njia tofauti na wengine wao walipata adhabu ya papo kwa papo ambapo leo inaweza isionekane adhabu hiyo.

"Lakini ikapatikana adhabu ya kiuchumi, uchumi ukadorora, hali ikawa ngumu ya maisha, shida ikatesa watu, watu wakakosa furaha na amani.

"Lakini, Mungu akamnyanyua Mwinjilisti wa Kimataifa Alphonce Tamba ayaeleze nini kinatakiwa kufanyika ili kuwe na amani na utulivu.

"Halafu kwa kutokujua kwa wananchi au watu wa Taifa hilo wakaingia kwenye mitandao kumbeza na kumdhalilisha, kumtukana, kumdhihaki, matokeo yake ni nini?.

"Wanaofanya hivyo ukiwachunguza katika mwenendo wa maisha yao watajikuta wanatembea katika laana ya kifamilia, laana ya ubinafsi kwa sababu walipambana na sauti ya Mungu aliyoileta pawepo na uponyaji na wao wakawa kinyume,"amesema.

Hivyo anasema ndiyo maana inatakiwa ukae makini kushindana na watumishi wa Mungu kwani imeandikwa msiwaguse wapakwa mafuta wa Mungu, kwa maana ya watumishi wa Mungu wenye kazi mbalimbali za Mungu duniani.

Kwamba kwa kuwa kwa sasa utii kwa Mungu duniani kutokana na teknolojia kuongezeka umeshuka kwa kiasi kikubwa, Dunia isitegemee kuona mambo mazuri yakitokea katika masiha yao kwani hata huko Ulaya na Marekani, uchumi kwa sehemu kubwa ni mzuri kupita maelezo na wamejipanga vizuri lakini bado wakirudi katika nagazi ya familia utakuta wana matatizo makubwa kuliko hata familia za Afrika.

"Matatizo ya madawa ya kulevya yanazidi Afrika, matatizo ya kuuana kwa kutumia silaha yanazidi huku Afrika pamoja na nchi zao kuwa na amani kubwa ambayo wana uwezo mkubwa wa Serikali kutumia Jeshi la Polisi kuwalinda wananchi wake na kuwahi katika matukio mbalimbali kwa wakati.

"Lakini bado kuna nguvu ya ndani ya kiroho ya uovu ambayo inawatesa, matokeo yake Serikali imekua ikipanga bajeti kubwa kwenye nchi mbalimbali za Ulaya kwa ajili ya kupambana na haya magenge yanayoharibu mataifa yao, pasi kujua kabisa mambo yale kwa kumheshimu na kumsikiliza Mungu, yangeweza kuisha kabisa," anaeleza Mwinjlisti Temba.

Anaeleza kuwa, moja ya sababu ya aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump kutaka kurudi madarakani ni kwa sababu pamoja na kwamba yupo na madhaifu mengi, lakini amekuwa katika kinywa chake akimheshimu Mungu kuliko Rais yeyote aliyewahi kuiongoza Marekani akitamka hadharani kwamba kwa kitendo hicho kinaweza kikasafisha mabaya yote yaliyoonekana kwake, kwa kusema ama kufikirika ndani yake na hivyo Mungu akamrudishia Kiti cha Urais wa Marekani.

Anasema, ndipo basi Dunia inaweza kushangaa namna gani Trump amekuwa Rais pamoja na kwamba Serikali ya Joe Biden imefanikiwa kumwekea vikwazo na vizuizi vingi kuliko mtu yeyote aliyewahi kugombea urais duniani kwa kumfungulia kesi zaidi ya 100 na kuendelea kudhalilishwa katika mitandao ya Kimataifa na ya jawaida katika nchi ya Marekani.

"Na bado mtu huyo akapenya, akawa Rais, kwa sababu Trump anadhalilishwa mpaka ndani ya chama chake kwa baadhi ya wagombea wenzake wanaosaka tiketi ya kugombea Kiti cha Urais na wanachama.

"Lakini,kwa sababu anamuheshimu Mungu hadharani Mungu anafanya mambo makubwa katika maisha ya mtu ama kiongozi kama huyo. Huu ni mfano halisi naweza kuwaeleza," anabainisha Mwinjilisti Temba.

Akizungumzia kuhusu watumishi ambao wana 'Fullness of God' anasema, kuwatambua ni neema kwani wanaweza wakaishi maisha ya kawaida akitolea mfano Yohana Mbatizaji ambaye alikuwa akiishi maisha ya kawaida akivaa ngozi na kula nzige na asali na kulala maporini, lakini maandiko yanazungumza kuwa ndiye mtumishi mkuu kuliko watumishi wote katika kitabu cha Agano Jipya.

"Hakuna mtumishi aliyekuwa mkuu kama yeye katika Agano Jipya, ndivyo maandiko yanavyosema ni Mkuu kuliko watumishi wote,".

Hivyo Mwinjilisti Temba anasema kuwa leo hii Dunia inahitaji vipawa na karama za Mungu viheshimiwe na viongozi, vitambuliwe na Watu, Mungu aendelee kutenda miujiza yake katika Mataifa, kwamba kwa kutokufanya hivyo Mungu ataruhusu adui yako akutese, ataruhusu, matatizo, majanga juu ya Taifa lako na uteseke.

Anasema, lengo ni ili katika kuteseka kwako ulitaje jina lake kwa kuomba rehema, kwamba ndipo mataifa mengi hususan ya Afrika yanapokwenda ambapo yamekosa watumishi wengi wenye macho ya Kiroho ambao Mungu amewapa neema hiyo kwasababu sio kila mtumishi, Nabii anayeweza kuyaona mambo yote ya Serikali na kupewa maelekezo na Mungu aeleze nini cha kufanyika.

"Unaweza ukawa Nabii Mkubwa sana, lakini ukawa huna neno juu ya Serikali yako, na ndivyo Manabii wengi walivyo, kwahiyo ni Manabii wachache sana, wakati Yohana Mbatizaji alivyomuonya mfalme kilichompata, kichwa kilikatwa pamoja na ukuu wake wote, kichwa kilikatwa kwa ombi la Mwanamke, utaweza kuona ni namna gani ukuu aliokuwa nao lakini mwisho wa siku kifo chake kilikuwa ni cha aibu na cha ajabu sana.

"Nachoweza kusema hivi sasa, mataifa mbalimbali na Tanzania, Watanzania wamuhofu Mungu, wamtangulize Mungu mbele, wamsikilize Mungu, katika Kitabu cha Kumbukumbu la Torati 28, kiko wazi watu wakiitii sauti ya Mungu na kumuheshimu Mungu watabarikiwa mjini, watabarikiwa vijijini, hazina za nchi zitabarikiwa na mambo hayo hayo yanazungumzwa kuanzia mlango wa 15.

"Wakienda kinyume Bibilia imesema maneno mengi sana, mapigo, magonjwa yasiyojulikana, watoto kuolewa na kuachika, wake za watu kuachika, kuchukuliwa hovyo na watuwengine, maisha kuwa magumu, matatizo ya kila aina, maradhi ya kila aina hulipata Taifa husika kwasababu ya kutokumtii Mungu na kumheshimu,".

Kwa hiyo anasema tunaweza tukaona hali ya kisiasa, hali ya upinzani, hali ya maisha magumu, hali ya matatizo, tukaona na tukasema vitu vingi ikiwemo kutaja majina, tukalaumu vyama, Rais na wataalamu, na mawaziri wakafukuzwa kila wakati na matatizo yakaja ya umeme, ya magonjwa na tukaangalia katika macho ya kibinadamu, lakini yupo mtu anayeyaona tofauti na watu wengine wanavyoona.

Kwamba na Watanzania wote wanaweza kufanya maombi na Mungu asijibu na hali ikazidi kuwa mbaya akitolea mfano Eliya alivyofunga Mvua kwa miaka mitatu na nusu, kwamba Bibilia inasema kulikwa na manabii zaidi ya 7,000 ambao kazi yao ilikuwa ni kuomba, lakini Mungu hakuwajibu Manabii hao kwasababu aliyeifunga alikuwa bado yupo hai, mpaka ilipofika wakati wake baada ya miaka ile aliyoisema ikafunguliwa na yeye mwenyewe.

"Kwa hiyo kuna neno ambalo Mungu ameliweka ndani ya Mtumishi wake Mwinjilisti wa Kimataifa Alphonce Tamba akilisema Tanzania hakuna mtu wa kulifungua mpaka mimi mwenyewe nirudi kulisema.

"Sasa hiyo ni neema, kutambua hilo ni neema kwa sababu pia kuna ufahamu wa kimungu mpaka uwe nao ndiyo ujue, lakini maandiko yamenena na kwa kuwa maandiko yamenena hatuwezi kupingana na maandiko, kwa sababu anayefanya yote haya ni Mungu, kwa kusudi lake Mungu.

"Sio kwa kusema Mungu hapa anatupenda kuliko watu wengine, haiwezekani Mungu akawapenda Watanzania pekee kuliko kuwapenda Wakongo.

"Haiwezekani Mungu akawapenda pekee Watanzania kuliko kuwapenda Wasomali, haiwezekani Mungu akawapenda Watanzania kuliko kuwapenda Wasudan, haiwezekani Mungu kuipenda Tanzania kuliko kuipenda Jamhuri ya Afrika ya Kati.

"Haiwezekani Mungu akaipenda Tanzania kuliko Nigeria, haiwezekani ule ni ufahamu mdogo sana wa kumjua Mungu, kwasababu watu hawajui kwanini vyanzo vingi vya matatizo katika mataifa ni nini,"amesema.

Mwinjilisti Temba amevitaja vyanzo vya matatizo katika mataifa mengi kuwa ni uovu na uasi mbele za Mungu na kukosekana kwa rehema, lakini wako watu wanaofanya hivyo kutokana, ama watumishi waliokwenda wakadharaulika ama kwa kutokutii kwa Taifa kumeyasababisha hayo, ndipo Mungu hunyanyua watumishi wake na kuishi katika maisha yoyote kwa utukufu wa Mungu, lakini wakawa na kipawa kikubwa cha kubadilisha hali.

Hata hivyo anasema, shida iliyopo ni kwamba utambuzi na kujulikana kwake kwa Mataifa ni mdogo, ndiyo maana mataifa yanaangamia. Kwasababu hiyo Mwinjilisti wa Kimataifa Temba anaeleza kwa kuwa Mungu alimtuma Kenya na kipindi cha Corona akiwa nchini Botswana aliwakuta Wabotswana wakiwa 'Lock down' na ndiyo nchi iliyokuwa ya mwishoni kuathirika ambapo aliishauri Serikali ya Botswana kufanya maombi na hivyo ikatangaza maombi ya mwezi mzima na kwamba baada ya mambo hayo Corona ikawa imefutika yenyewe na watu wakaachiliwa.

"Mungu amenituma Zambia tangu kipindi cha Rais Levy Mwanawasa, nikamkuta Mwanawasa akiwa madarakani ni kazungumza na wasaidizi wake hususan na aliyekuwa mshauri wake wa masuala ya Dini 2004, nikamwekeza wazi juu ya matatizo yatakayomkuta Mwanawasa endapo nisingemuombea.

"Nikamweleza wazi atashinda uchaguzi wa mwaka 2006, lakini hatakaa madarakani atafariki, pamoja na mjadala mrefu nilitumwa niende kwenye ubalozi wa Zambia nchini Tanzania nipelekea Barua nielezee kisa cha kumuona Rais kwasababu ilikuwa ni maneno magumu, nikaenda nikafanya hivyo,"amesema Mwinjilisti.

Kwamba pamoja na kufanya hivyo Ubalozi wa Zambia nchini Tanzania ulihitaji kupata baadhi ya watumishi wanaomfahamu Mwinjilisti Alphonce Temba ili kwenda kujiridhisha kama kweli ni Mtumishi wa Mungu au ni mtu anayefanya ujanja ujanja.

Hivyo Mwinjilisti Temba anabainisha kuwa, hakusita kumtaja Mtumishi wa Mungu Mchungaji Deo Lubala aliyekuwa na kanisa lililoitwa World Alive lililokuwa Sinza na ndipo Balozi na Wasaidizi wake wakaenda katika kanisa la Deo Lubala huku bendera ya Zambia ikipepea kwenda kutafuta habari za Mtumishi wa Kimataifa Temba kama ni kweli ni Mtumishi wa Mungu, kwani ujumbe huo uliwafanya wasiweze kutulia ofisini.

Anasema, walipofika Mtumishi wa Mungu, Deo Lubala alizungumza nao na kuwaeleza kuwa Mwinjilisti Temba yupo na anafahamika na ni mtumishi wa Mungu, kwamba baada ya kuwajibu hivyo walirudi na barua kuituma Zambia, lakini haikufanyiwa kazi na baada ya mwaka mmoja Rais Mwanawasa alishinda uchaguzi na muda mfupi uliofuata Rais Mwanawasa alifariki dunia.

"Na ndipo Mungu akarudi kwangu (Mwinjilisti wa Kimataifa Alphonce Temba), akanionyesha Mwenyekiti wa PF Michael Sata, nikapewa unabii juu yake kwamba atakuwa Rais, unabii huo nilipewa 2007, na niakenda nikawasiliana naye kwani kwa njia za kimungu nilipata mawasiliano yake nikawasiliana naye nikampa unabii huo pamoja na kwamba Sata alikuwa akiitwa King Cobra Mkatoliki mwenye msimamo mkali asiyekubaliana na vuguvugu la Wapentecoste, lakini alivyoisikia sauti yangu Mungu akaugeuza moyo wake akatii akakubalina na sauti hiyo," anasimulia Mwinjilisti Temba.

Kwamba tangu alipopata unabii huo mwaka 2007, ulikuja kutimia baadaye kwani Sata alishinda Uchaguzi Mkuu na kuwa Rais, hivyo anaeleza kuwa kuyajua na kuyakubali hayo bila kuwa na neema ya Mungu ndani yako inakuwa ni ngumu sana na ndicho kinachoangamiza viongozi na watu wengi duniani na hiyo ni kwasababu ya kubeba viashiria vya viburi katika mioyo ya watu na kudharau.

Kwamba wakati akiwa nchini Botswana, Mwinjilisti wa Kimataifa Temba, anasema Mungu alimtokea na kumwambia kuwa atamtuma katika mataifa mbalimbali na kumweleza kuwa ataanza na nchi ya Tanzania na Zambia na kwamba atatamka mambo makubwa ambayo yatakwenda kuponya mataifa hayo.

Alielezwa kuwa atatabiri juu ya watu kuwa Marais na kuombea uchumi wa nchi hizo, ndani na nje Afrika, lakini alielezwa kuwa atakuwa na vikwazo vitakavyomtaka awe mvumilivu ikiwemo kudharaulika.

"Na ndiyo maana siku zote katika mambo ninayoyafanya, nimekuwa mvumilivu juu ya dharau, na nimekuwa sipambani wala kugombana na watu, kwasababu nilikwishaelekezwa kwa kuwa Mungu aliniambia Taifa lolote litakaloniheshimu litafanikiwa, nikaambiwa pia asilimia kuwa ya watu watakaonidharau, watakuwa ni watumishi wa Mungu, hivyo uwe mvumilivu, ushuhuda huu mzinto ambao kwa mara ya kwanza nimeuelezea umekuwa ni ushuhuda mkubwa sana ambao ni wakusisimua, hakika Mungu anao watu wake waliojificha,".

Mwinjlistia Temba anasema kuwa anaendelea kumshukuru Mungu kwa yote aliyomuonyesha tangu mwaka 2003, 2004 alivyomtoa Tanzania na kumpeleka Botswana kwa miaka mitano na kumfundisha, na kuwaomba watu waendelee kumfuatilia kwani kuna mambo makubwa na magumu yatakayotokea Duniani na kwamba ataendelea kuyasema kwani hata TB Joshua aliwahi kumtabiria mambo makubwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news