Ofisi ya Kikosi cha Zimamoto na Uokozi Kanda ya Kaskazini huko Mahonda yazinduliwa

ZANZIBAR-Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi,Mhe. Rahma Kassim Ali amesema Serikali itaendea kuvijengea uwezo vikosi vya ulinzi na usalama nchini ili viendelee kulinda wananchi na mali zao.
Akizungumza katika Uzinduzi wa Ofisi ya Kikosi cha Zimamoto na Uokozi Kanda ya Kaskazini huko Mahonda amesema, Serikali imejenga majengo bora na vifaa wezeshi ili vikosi hivyo vizidi kufanya kwa kazi kwa ufanisi.

Amesema kuwa, ujenzi wa jengo la ofisi hiyo umezingatia mahitaji ya kikosi hicho katika Kanda hiyo ambayo ina uwekezaji mkubwa kwa lengo la kukabiliana na majanga mbalimbali pale yanapojitokeza.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja, Rashid Hadid Rashid amekipongeza kikosi hicho kwa uaminifu wanaouonesha katika ujenzi wa miradi mbalimbali nchini.

Mradi wa Ujenzi huo umesimamiwa na Kikosi cha Zimamoto na Uokozi na kugharimu shilingi milioni 880 hadi kukamilika kwake.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news