KIGOMA-Samahani, mimi naitwa EMMANUEL YAKOBO KALIMUNDA, Mawasiliano yangu ya simu ni 0766153840/0622304638.
Mimi ni mzaliwa wa Kijiji cha Kaseke Juu, Kata ya Simbo, Wilaya ya Kigoma, Mkoa wa Kigoma, kwa sasa naishi Wilaya ya Kasulu kikazi.
Tafadhali, lengo la ujumbe huu ni kutafuta msaada wa mjomba wangu huyu kwenye picha anayeitwa ASIA REHANI anayeumwa huo ugonjwa kama anavyoonekana.
Hivyo, kutokana na hali ya kiuchumi ya familia na changamoto ilivyokubwa kiukweli imeshanizidi nguvu kabisa maana mimi ndio ninapambana na hiyo changamoto kwa kuomba michango kwa watu mbalimbali toka mwezi wa nne mwaka 2023 mpaka hivi leo.
Tumejaribu njia mbalimbali, tumempeleka kwenye huduma za hospitali, kwenye huduma za maombezi n.k bila mafanikio.
Wakati mwingine hospitali walikuwa wanasema hana ugonjwa wowote yaani vipimo havionyeshi tatizo ni nini, ingawa baadhi ya ULTRASOUND ziikuwa zikionyesha anavidonda vingi vinavyoanzia tumboni.
Majibu ya ugonjwa huu yamekuwa tofauti tofauti mpaka tumeshindwa kujua ni nini shida maana kuna wanaosema huu ugonjwa unaitwa TEN ambapo dawa yake ni sindano na amechomwa sana bila mafanikio, wengine wakasema ni VITIRIGO ambapo huduma yake inasadikika haipo na kadhalika.
Hivyo, naomba msaada wa Serikali na wadau wasamaria wema wanisaidie kumtibu huyu mjomba wangu.
Tumeshahangaika, nimeuza kila kitu kwa ajili ya kumtibu, lakini hali inazidi kuwa mbaya tu. Sina hata uwezo wa kumhudumia chakula kwa sasa.
Emmanuel Kalimunda.