Prof.Muhongo awaita wadau Shule Shikizi ya Kiunda

NA FRESHA KINASA

WANANCHI na wadau wa maendeleo katika Jimbo la Musoma Vijijini mkoani Mara, wameombwa kujitokeza kushiriki katika harambee ya kuchangia ujenzi wa miundombinu ya elimu kwenye shule Shikizi ya Kiunda ya Kijiji cha Kamguruki jimboni humo.

Harambee hiyo, itafanyika Ijumaa ya Januari 12, 2024 majira ya saa nane mchana katika Kitongoji cha Kiunda Kijijini Kamguruki.

Ikiwa ni jitihada za Mbunge wa Musoma Vijijini Prof. Sospeter Muhongo na Wananchi jimboni humo kuendelea kushirikiana kuimarisha sekta ya elimu na kuhakikisha Watoto hawatembei umbali mrefu kwenda masomoni.

Hayo yamebainishwa Januari 6, 2024 kupitia taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo hilo chini ya Mheshimiwa Prof.Sospeter Muhongo, "Shule Shikizi Kiunda inajengwa kwenye Kitongoji cha Kiunda kijijini Kamguruki, Kata ya Nyakatende.

"Shule hii inatayarisha watoto wa vitongoji vitatu kwenye masomo ya awali, baadaye watoto hao wanaenda kuanza masomo ya Shule ya Msingi mbali na nyumbani kwao, tatizo la umbali mrefu wa kwenda masomoni.

"Wote tunakarabishwa kuchangia ujenzi wa shule hii kwa kushiriki harambee iliyoelezwa, au kutuma mchango wako moja kwa moja kwenye Akaunti ya Kijiji cha Kamguruki;

Akaunti ya Benki:
Benki: NMB
Akaunti Na: 30302300679
Jina la Akaunti: Kijiji cha Kamguruki.
Karibu tuboreshe elimu Vijiji mwetu.
Picha ya inaonesha hatua iliyofikiwa kwenye ujenzi wa miundombinu ya elimu kwenye Shule Shikizi Kiunda ya Kijijini Kamguruki, Musoma Vijijini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news