Rais Dkt.Mwinyi afanya mabadiliko Baraza la Mapinduzi, ateua Mawaziri

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amefanya mabadiliko ya Barazala Mapinduzi kwa kuteua mawaziri wawili wawili na kumbadilisha wizara waziri mmoja.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Zena A.Said ambapo uteuzi huo umeanza Januari 27,2024.

Rais Dkt.Mwinyi amefanya mabadiliko ya Baraza la Mapinduzi kwa kuteua Mawaziri wapya wawili na kumbadilisha Wizara Waziri mmoja ambapo ameteua Mudrik Ramadhan Soraga kuwa Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale akichukua nafasi ya Simai Mohammed Said ambaye amejizulu.

Pia,Rais Dkt. Mwinyi amemteua Ali Suleiman Ameir (Mrembo) kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Ikulu huku akimteua pia Shaaban Ali Othman kuwa Waziri wa Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi.

Juma Makungu Juma ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango,  Salha Mohamed Mwinjuma ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi na Zawadi Amour Nassor ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Maji, Nishati na Madini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news