ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi ametoa shukrani kwa Kamati ya maandalizi ya sherehe za miaka 60 ya Mapinduzi mwaka huu chini ya Makamu wa Pili wa Rais, Mhe.Hemed Suleiman Abdullah kwa uratibu mzuri.
Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo usiku wa kuamkia leo Januari 22,2024 alipojumuika na wachezaji, viongozi wa timu ya Mlandege katika hafla ya chakula cha usiku alichowaandaliwa Ikulu jijini Zanzibar.
Aidha, Rais Dkt.Mwinyi ameipongeza Kamati ya Mapinduzi Cup chini ya Mbarouk Suleiman Othman, pia amewashukuru wadhamini mbalimbali wa mashindano hayo.