ZANZIBAR-Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amekubali ombi la kujiuzulu kwa Simai Mohamed Said, aliyekuwa Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, Mhandisi Zena A.Said imesema, Rais Dkt.Mwinyi ameridhia ombi hilo kuanzia leo Januari 26, 2024.
Hayo yanajiri ikiwa ni muda mfupi tangu Waziri Simai atoe taarifa kuwa anaachia nafasi hiyo.