Rais Dkt.Mwinyi atimiza ahadi ujenzi wa Kiwanda cha Mwani Zanzibar

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema kukamilika kiwanda cha kusarifu Mwani Chamanangwe kitakuwa na uwezo wa kununua tani 30,000 za Mwani kwa wakulima.
Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo Januari 5,2024 alipoweka Jiwe la Msingi Kiwanda cha kusarifu Mwani Chamanangwe Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Aidha, Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa kiwanda hicho kitapokamilika ajira zitapatikana, bei itapanda pamoja na soko la uhakika la nje kutokana na kusarifu hapa nchini.
Halikadhalika Rais Dkt.Mwinyi amesema Serikali itaendelea kuwawezesha Wakulima wa Mwani kwa kuwapatia maboti , mashine pamoja na zana mbalimbali za kuzalisha Mwani ili kuongeza uzalishaji kwa wingi wa Mwani.
Kwa upande mwingine Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa kujengwa kiwanda hicho ambacho ni kikubwa Afrika inatokana pia kuwa Zanzibar ni nchi inayoongoza kwa kuzalisha zao hilo Afrika.
Vile vile amesema kuwa Mikoa ya Tanzania Bara ya mwambao ikiwemo Mtwara, Tanga wako tayari kuuza Mwani Zanzibar.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news