Rais Dkt.Mwinyi aweka jiwe la msingi hoteli ya nyota tano ya Zanzibar Crown Mazizini

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema sheria mpya ya uwekezaji ya mwaka 2023 itakuwa bora Afrika ambayo ataisaini hivi karibuni baada ya kupitishwa na Baraza la Wawakilishi mwezi Novemba mwaka jana.
Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo leo Januari 7,2024 alipoweka jiwe la Msingi la ujenzi wa Hoteli ya nyota tano ya Zanzibar Crown Mazizini, Wilaya ya Magharibi B Mkoa wa Mjini Magharibi.

Aidha,Rais Dkt.Mwinyi amewapongeza wawekezaji wa hoteli hiyo kwa kuwekeza dola za kimarekani milioni 30 kwa mradi wa hoteli ambapo utatoa fursa ya ajira ya Wazanzibari zaidi ya 200.

Halikadhalika Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa lengo la Serikali ifikapo mwaka 2025 kupokea watalii milioni moja ambapo sasa Zanzibar inapokea watalii laki tano na elfu sitini kwa mwaka.
Vilevile Rais Dkt.Mwinyi amesema Zanzibar inaongoza kupokea ndege nyingi Tanzania kwa sasa ukilinganisha na viwanja vya ndege vya Kilimanjaro na Dar es Salaam .

Kwa upande mwingine Rais Dkt.Mwinyi amewapongeza wawekezaji hao kwa uamuzi wa ujenzi wa soko la kisasa la wavuvi na Msikiti pembezoni mwa hoteli hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news