Rais Dkt.Mwinyi azidi kuipaisha Zanzibar, Sekta ya Elimu mambo safi

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali inakaribia kumaliza ujenzi wa madarasa 5,000 ili kuondoa zamu mbili kwa wanafunzi nchi nzima na kubakisha zamu moja.
Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo Januari 9,2024 alipofungua rasmi Skuli mpya ya Sekondari Tumekuja iliyopo Mwembeladu Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi katika shamrashamra za Miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Vilevile Skuli hiyo mpya ya Tumekuja ina uwezo wa kuchukua wanafunzi 1,755 kwa wastani wa uwiano wa wanafunzi 45 kwa darasa moja, tayari wanafunzi wameshapangwa wiki ijayo kuanza masomo.
Rais Dkt.Mwinyi amempongeza mkandarasi wa kampuni ya CRJE kwa kujenga Skuli ya kisasa ambayo ina maabara tatu ya kisasa, chumba cha kompyuta, maktaba na ukumbi wa mikutano.

Aidha Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa Serikali itaendelea kujenga maghorofa katika sekta ya elimu kwa wanafunzi kutozidi 45 kwa darasa moja .

Halikadhalika Rais Dkt.Mwinyi amesema Serikali itaendelea kufanya uamuzi sahihi kwa faida ya nchi na kuyakarabati majengo ya mji mkongwe kwani ni urithi wa nchi kwa manufaa ya vizazi vijavyo.
Kwa upande mwingine Rais Dkt.Mwinyi amesema mafanikio yaliyopatikana katika elimu ni kwa juhudi za Waalimu kwa kuongeza idadi ya ufaulu ikiwemo kutoka wanafunzi 2,000 hadi 6,000 Skuli za Msingi na matokeo ya kidato cha sita ya mwisho ufaulu wa daraja la kwanza hadi daraja la tatu kwa asilimia 90.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news