Rais Dkt.Mwinyi azindua jezi za Zanzibar Heroes

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema, jezi alizozindua zitatumika katika mashindano ya uwakilishi wa nchi ndani na nje katika michuano ya madaraja mbalimbali.
Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo Januari 26,2024 alipozindua rasmi Jezi za Timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) katika Viwanja vya maonesho Nyamanzi Mkoa wa Mjini Magharibi.

Aidha, Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa,changamoto ya Zanzibar kushiriki michuano inayoandaliwa na Shirikisho la mpira Afrika (CAF) ikiwemo michuano ya AFCON inaelekea kupatiwa ufumbuzi kupitia Wizara ya Michezo kwa kushirikiana na Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF).
Kwa upande mwingine Rais Dkt.Mwinyi amempongeza mbunifu wa mavazi nchini Sheria Ngowi kwa ubunifu wa jezi hizo.

Pia ameishukuru Benki ya CRDB kwa kuona umuhimu kuunga mkono jitihada za Serikali katika michezo.
Vilevile Serikali inayo azma ya kufundisha makocha nchini pamoja na kuhamasisha uendelezwaji na kuanzishwa kwa academia za michezo katika kuandaa timu bora ya Taifa kwa uwakilishi wa Kikanda na Kimataifa.
Halikadhalika Rais Dkt.Mwinyi ametoa wito kwa taasisi zinazolinda haki miliki kulinda jezi hizo pia kuchukua hatua za kisheria kwa mtu yeyote atakayebainika kutengeneza jezi hizo bila ridhaa au kibali maalum kutoka ZFF.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news