Rais Dkt.Mwinyi:Elimu ni kipaumbele namba moja

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali imeweka kipaumbele namba moja katika sekta ya elimu imeongeza bajeti kutoka shilingi bilioni 265 mwaka 2021 hadi shilingi bilioni 457.
Amesema, lengo ni kuongeza juhudi katika sekta hiyo kwa ujenzi wa miundombinu ya kisasa ikiwemo Skuli za msingi na Sekondari za ghorofa zinazojumuisha maabara za kisasa, maktaba na vyumba vya kompyuta.
Rais,Dkt.Mwinyi amesema hayo Januari 7,2024 alipofungua Skuli ya kisasa ya Msingi Fuoni Wilaya ya Magharibi B, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Aidha, Skuli hiyo ya mfano ya kisasa imejengwa kwa miezi mitano na kampuni ya ROK Development B.V ya Uturuki na kusimamiwa na Wakala wa Majengo ya Serikali (ZBA) ambayo ni aina ya ghorofa mbili kwa ujenzi wa teknolojia ya PRE FABRICATION kwa fedha za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar shilingi bilioni 7.8.
Halikadhalika Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa Serikali itaendelea kuajiri walimu wa fani zote hususani wa masomo ya sayansi na hesabu ili waweze kutoa elimu bora na kwa mwaka huu itaajiri walimu 1,500.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news