Rais Dkt.Mwinyi:Tunajenga bandari mpya ya abiria eneo la Mpiga Duri

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema ujenzi wa bandari mpya ya abiria eneo la Mpiga Duri ni azma ya Serikali kuondoa msongamano katika bandari ya Malindi sehemu ya abiria ambayo ina changamoto ya nafasi.
Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo Januari 9,2024 katika hafla ya utiaji saini mkataba wa ushirikiano kati ya Serikali na kampuni ya ZF DEVCO ya ujenzi wa bandari ya abiria eneo la Mpiga Duri, Ikulu jijini Zanzibar.

Aidha, Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa bandari hiyo ya kisasa itakuwa na eneo la boti za abiria, usafiri wa boti za mizigo, taxi za baharini, maduka ya kisasa, ndege zinazotua na kuruka baharini, kituo cha umma cha mabasi, hoteli ya nyota tano, ukumbi wa kimataifa wa mikutano pamoja na eneo la maegesho ya boti.

Vilevile gharama za mradi wa ujenzi huo ni dola za kimarekani milioni 400, na utakamilika kwa miezi 36 ijayo.

Hafla hiyo imehudhuriwa na Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania Mhe. Wiebe De Boer, Viongozi mbalimbali wa Serikali na Vyama vya siasa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news