DAR ES SALAAM-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua aliyewahi kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Dkt. Athuman Kihamia kuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART).
Dkt.Kihamia anachukua nafasi ya Dkt. Edwin P. Mhede ambaye uteuzi wake umetenguliwa na atapangiwa kazi nyingine.
Wakati huo huo, Mheshimiwa Rais Dkt.Samia amemteua Musa Kuji kuwa Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Kuji alikuwa akikaimu nafasi hiyo.