NA DIRAMAKINI
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Bi. Doris Ntuli Kalasa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa.
Kabla ya uteuzi huu Bi. Kalasa alikuwa Afisa Mwandamizi Ofisi ya Rais-Ikulu na anachukua nafasi ya Mhandisi Leonard Robert Masanja ambaye amestaafu.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Januari 18, 2024 na Zuhura Yunus ambaye ni Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu.