Rwanda hatupelekeshwi na yeyote-Rais Kagame

KIGALI-Rais wa Jamhuri ya Rwanda, Mheshimiwa Paul Kagame amesema, hakuna chombo chochote kutoka nje ya nchi hiyo ambacho kinaweza kuiamuru Rwanda njia ipi ipite.
Vile vile kuuamuru uongozi juu ya nini cha kufanya, kwani jukumu hilo ni la watu wa Jamhuri ya Rwanda wenyewe tu.

Rais Kagame amesema hayo Januari 14,2024 jijini Kigali katika hafla ya 29 ya Maombi ya Kitaifa chini ya mada "Kutumikia watu wa Mungu kwa mabadiliko ya kudumu".

Mahubiri yalitolewa na Mchungaji Dkt. Goodwill Shana, Mwanzilishi na Mchungaji Mkuu wa Word of Life International Ministries.

"Imani, kwa maoni yangu, imani ambazo watu wanazo ni za aina tofauti, zinapaswa pia kutuimarisha sisi wenyewe.

"Zinapaswa kututia nguvu katika kuamua, katika kuchagua, katika kuamua ni nini kilicho bora kwetu.

"Na kukataa kuwa, watu wana haki ya kuja na kuamua kwa ajili yako, na kuamua hata kile kinachotokea kwako. Kataa tu.

“Watu wote tupo sawa mbele za Mungu hakuna Mtu ambaye yupo juu kuliko mwingine, ukweli huu uwe chanzo cha kuwapa hamasa na msukumo utakaowapa mwongozo wa matendo yenu kwenye masuala mbalimbali.

“Kwa kuizingatia historia ya Rwanda, changamoto tunazozipitia sasa na malengo yetu ya baadaye, ni dhahiri kwamba hakuna chombo chochote kutoka nje bila kujali asili yake ambacho kinaweza kutuamrisha njia ipi nchi yetu ipite, kutuamrisha uongozi wetu uweje na wapi tuelekee, jukumu hilo ni letu sisi watu wa Rwanda wenyewe,amefafanua Mheshimiwa Rais Paul Kagame.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news