Ofisi ya elimu Wilaya ya Mkoani Pemba yafunguliwa

ZANZIBAR-Mapinduzi ya Zanzibar ya Mwaka 1964 yalilenga kuondosha utawala wa kidhalimu na kuwafanya Wananchi kufurahia matunda ya Uhuru.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Mifugo na Maliasili,Mh. Shamata Shaame Khamis katika hafla ya Ufunguzi wa Ofisi ya Elimu Wilaya ya Mkoani, ikiwa ni Shamra shamra za maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Amesema katika kupiga Hatua kimaendeleo suala la Elimu ni Muhimu Hivyo Serikali imekua ikiimarisha miundombinu ya kielimu ili kusukuma mbele kasi ya maendeleo nchini.

Amesema, kutokana na Jitihada za Serikali za kutatua changamoto za kielimu Mafanikio yanaonekana ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa ufaulu katika ngazi mbali mbali.

Nae Naibu Waziri wa Elimu Na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mh. Ali Abdulghulam Hussein amesema zaidi ya Skuli 62 za ghorofa zimejengwa katika kipindi cha miaka mitatu ya Uongozi wa Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi.

Amesema Ofisi za Wilaya ni Mkakati katika Utekelezaji wa mageuzi makubwa ya Elimu yanayolenga kuimarisha ubora wa huduma za Elimu Nchini.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Bw. Khamis Abdullah Said akisoma taarifa ya kitaalamu ya Ujenzi wa Ofisi hiyo amesema Jumla ya Tsh. milioni 182 zimetumika takika ujenzi wa Ofisi hiyo ambayo lilianzishwa na Baraza la Mji Mkoani.

Amesema Wizara inamatunaini makubwa kwamba Kasi ya Ufuatiliaji itaongezeka kutokana na uwepo wa Ofisi hizo ambazo zimeshajengwa katika Wilaya.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news