Simba SC yaweka mambo hadharani

DAR ES SALAAM-Uongozi wa Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam umesema, malengo yake ni kujenga timu imara ambayo itakuwa na uwezo wa kushinda makombe.
Hayo yamesemwa leo Januari 21, 2024 na Afisa Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Imani Kajula katika Mkutano Mkuu wa Klabu ya Simba 2023 ambao unafanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

"Malengo ya klabu ni kujenga timu imara yenye uwezo wa kushinda makombe, kujenga taasisi imara na endelevu, kujenga chapa imara ndani na nje, ya Tanzania.

i"Kujenga misingi imara na yenye tija kwa wanachama na wapenzi, kujenga uwezo wa kifedha ili kufikia malengo, kuvutia wafanyakazi wenye weredi, kujenga misingi imara ya mawasiliano na matawi na wanachama.

"Tumefanya maboresho makubwa kwenye benchi la ufundi tukianzia na kocha nadhani wote mnaona.

"Tumeboresha idara ya afya ya timu yetu, tuna madaktari bora sana.

"Lakini pia tumeimarisha timu ya vijana kwa kutafuta vijana kutoka maeneo mbalimbali nchini.

"Timu yetu ya wanawake imekuwa bora sana. Eneo lingine ni tumeimarisha uhusiano kwa kiasi kikubwa na wadhamini wetu.

"Sehemu nyingine kubwa ni kushinda Ngao ya Jamii mbili na kuwa mashabiki bora wa AFL. Simba ilileta Rais wa FIFA na kubwa zaidi kuitangaza Tanzania.

"Tunataka kuwa mabingwa wa ndani na nje ya uwanja. Tulianzisha WhatsApp channel wakawa wanatusema, lakini leo hii tunaongoza kwa kuwa namba moja Afrika Mashariki na Kati na walikuwa wametuzidi YouTube,lakini hivi ninapoongea sasa tumewapita na tunaongoza kwenye mitandao yote.

"Tutaendelea kujenga rasilimali za Simba na eneo lingine ni kuwa na wafanyakazi wenye weledi na uwezo mkubwa sana. Mbele tunaangalia kuboresha mapato, kuimarisha biashara ya jezi.

"Sandaland amefanya yale mliyokuwa mnayataka kama jezi kutoka mapema na jezi yenye ubora.

"Ni mzabuni aliyetimiza malengo yenu wanachama. Mwaka huu tunaangalia namna ya kushirikisha matawi katika uuzaji wa jezi ili kuwaongezea mapato.

"Changamoto zilizopo ni rasilimali fedha, kuongezeka kwa gharama za uendeshaji, kutanuka kwa mahitaji, kuumia kwa wachezaji, mabadiliko na ushindani kuongezeka na kuendelea kuwa timu namba moja,"amesema Imani Kajula.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news