Spika Dkt.Tulia,Jaji Mkuu watembelea banda la DCEA katika Wiki ya Sheria jijini Dodoma
DODOMA-Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson, na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mheshimiwa Prof. Ibrahim Hamis Juma wametembelea banda la Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA).
Viongozi hao wametembelea banda hilo Januari 27,2024 wakati wa hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Sheria inayofanyika kitaifa katika Viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma.
Wakiwa bandani, viongozi hao walielezwa jinsi mamlaka inavyofanya kazi zake katika kupambana na dawa za kulevya.
Hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Sheria imechagizwa na matembezi ya hisani ya kilometa 6 kwa viongozi na washirki wote wa maadhimisho hayo ambapo matembezi yalianzia Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma hadi katika Viwanja vya Nyerere jijini humo.