TAEC yataja umuhimu wa kudhibiti mionzi kwenye mnyororo wa bidhaa

ZANZIBAR-Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) imebainisha sababu na umuhimu wa kudhibiti mionzi kwenye mnyororo wa bidhaa.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa TAEC, Bw.Peter Ngamilo katika Maonesho ya Biashara yanayoendelea jijini Zanzibar.
Ofisi ya TAEC Kanda ya Kaskazini (Arusha).

Katika maonesho hayo,TAEC inashiriki kutoa elimu juu ya majukumu inayoyatekeleza kisheria ndani ya Jamhuri ya Muungano ya Muungano wa Tanzania.

Ngamilo amesema kuwa, zipo sababu nyingi zinazopelekea kudhibiti mionzi kwenye mnyororo wa bidhaa, lakini sababu chache na za msingi ni kuwa usafirishaji holela wa vyanzo vya mionzi unaweza kupelekea uchafuzi wa mionzi kwenye mnyororo wa bidhaa na hivyo kupeleka kuleta madhara ya magonjwa kama saratani endapo hakutakuwa na udhibiti wa kutosha.
Maabara changamana awamu ya pili iliyopo Kanda ya Kaskazini Arusha.

Sababu nyingine, Ngamilo amesema katika mazingira yetu kuna viasili vya mionzi kutokana na ukweli kwamba kwenye baadhi ya maeneo nchini kuna uwepo wa madini ya urani.

Amesema, hali hiyo inaweza kupelekea baadhi ya mimea inayolimwa katika maeneo hayo ikawa inafyonza mionzi na mwisho wa siku ikaleta madhara kwa walaji,hivyo ni muhimu kudhibiti kwa kupima sampuli za kimazingira kama vile udongo na maji.
Jengo la Ofisi na Maabara la TAEC Kanda ya ziwa (Mwanza).
Makao Makuu ya TAEC Dodoma.
Sambamba na mimea yenyewe ili kubaini kama ina mionzi ili kuendelea kulinda watanzania dhidi ya madhara ya mionzi na uchafuzi wake kwenye mnyororo wa bidhaa.

Pia, Bw.Ngamilo amesema kuwa, sababu nyingine ni jukumu la Serikali kulinda wananchi wake dhidi ya uchafuzi wa mionzi kwenye mnyororo wa bidhaa ndio maana Serikali inaendelea kuwekeza katika kufungua ofisi katika maeneo mbalimbali nchini kama vile maeneo ya mipaka.
Amesema kwa sasa TAEC ina ofisi 62 nchi nzima ambapo kati ya hizo Ofisi za Kanda ni 7, Kanda ya Kati (Dodoma na Makao Makuu), Kanda ya Mashariki (Dar es Salaam), Zanzibar, Kanda ya Kaskazini (Arusha), Kanda ya Ziwa (Mwanza).

Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, na Kanda ya Kusini na ofisi zingine 55 ziko mikoani na mipakani huku pia Serikali ikielekeza nguvu katika kujenga ofisi na maabara za kimkakati pamoja na kuziwekea vifaa vya kisasa katika kuhakikisha udhibiti na usimamizi wa matumizi salama ya mionzi unafanyika kwa umakini mkubwa.

Sababu nyingine ni katika kulinda masoko ya bidhaa za Tanzania nje ya nchi hivyo upimaji wa mionzi lazima ufanyike kwa umakini mkubwa kwa sababu vita vya kiuchumi ni vikubwa sana Duniani na isipofanyika hivyo inawezekana siku moja akatokea mtu ambaye hana mapenzi mema na nchini yetu akaweka mionzi kwenye bidhaa zetu na kupelekea kuonekana bidhaa za Tanzania zina mionzi hivyo zikakataliwa kwenye masoko ya nje.
Hivyo kupoteza kabisa uaminifu na kama ambavyo inafahamika kwa sasa Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan anatumia nguvu kubwa sana katika kufanya ziara nchi mbalimbalIlili kutafuta masoko na kuwaunganisha wafanyabiashara wa Tanzania katika masoko mbalimbali nje ya nchi.

Amesema, gharama inayotumia Serikali ni kubwa ili mradi tu mwisho wa siku watanzania waweze kunufaika na fursa hizo za kibiashara, hivyo hatuna budi kulinda masoko hayo kwa gharama yoyote ikiwemo uwekezaji wa vifaa vya kisasa vya kudhibiti mionzi.
Ofisi ya TAEC (Zanzibar).

Ni katika kuhakikisha bidhaa za vyakula zinapimwa kwa umakini mkubwa kabla hazijaenda kwenye masoko ya nje.

Ngamilo amebainisha kuwa, sababu nyingine ni kukidhi matakwa ya Sheria ya Bunge Na. 7 ya Mwaka 2003, ya Nguvu za Atomu na kanuni zake, pia kukidhi matakwa ya Sheria ya Shirika la Kilimo na Chakula Duniani (FAO), Shirika la Afya Duniani (WHO) na Wakala wa Kimataifa wa Nguvu za Atomu (IAEA).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news