Tanzania, Oman kuimarisha utamaduni na kumbukumbu

MUSCAT-Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Oman zimekubaliana kushirikiana kuimarisha sekta ya utalii kupitia utamaduni na kumbukumbu za mambo ya kale ili kuongeza utalii na kukuza uchumi wa mataifa hayo mawili kwa maslahi ya pande zote mbili.
Ahadi hiyo imefikiwa na Balozi wa Tanzania nchini Oman, Mhe. Fatma Rajab alipokutana kwa mazungumzo na Waziri wa Urithi wa Mambo ya Kale na Utalii wa Oman, Mhe. Salim Mohammed Al Mahrouq kujadili masuala mbalimbali ya kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Oman katika ukumbi wa Wizara hiyo.

Pamoja na mambo mengine, viongozi hao wamejadiliana na kukubaliana kuongeza fursa na ushirikiano katika nyanja za mafunzo na uzoefu kwa wataalam wa pande zote mbili. Adha, katika Utekelezaji wa mambo hayo, viongozi na wataalam wa Tanzania na Oman watakutana hivi karibuni kupanga mikakati ya utekelezaji wa makubaliano ya ushirikiano.

Mazungumzo hayo ni hatua ya utekelezaji wa Balozi wa Tanzania nchini Oman, Mhe. Fatma Rajab ya kukuza ushirikiano wa kidiplomasia na Utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news