DA ES SALAAM-Mikoa ya Morogoro, Lindi, Iringa, Mtwara, Mbeya, Songwe, Njombe na Ruvuma inatarajiwa kupata mvua za juu ya wastani.
Ni kuanzia Januari 30, 2024 ikiwa ni siku chache tangu mikoa ya Dar es Saalam na Morogoro ikumbwe na mafuriko.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ambayo imefafanua kuwa, mvua hizo zinaweza kusababisha athari kwenye miundombinu na makazi ikiwemo nyumba kuzungukwa na maji.
Sambamba na kuathirika kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi.
TMA imewataka wananchi kuchukua tahadhari na kujiandaa kwa dharura zinazoweza kujitokeza.