TRC yasitisha huduma ya safari za treni

DAR ES SALAAM-Shirika la Reli Tanzania (TRC) limetoa taarifa kuwa limesitisha kwa muda huduma ya safari za treni kutoka Dares Salaam kuelekea Mikoa ya Morogoro, Dodoma, Singida, Tabora, Katavi, Kigoma, Shinyanga na Mwanza.

Sambamba na mikoa ya Tanga, Kilimanjaro na Arusha kutokana na uharibifu wa miundombinu ya reli katika maeneo ya Mazimbu, Kilosa na Munisagara mkoani Morogoro, Godegode na Gulwe mkoani Dodoma.

Pia, maeneo ya Ruvu Junction, Wami, Mvave mkoani Pwani na eneo la Mkalamo Tanga kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
“Wahandisi kutoka TRC wanaendelea na matengenezo katika maeneo yaliyoathiriwa na mvua zinazoendelea na huduma ya usafiri wa treni zinatarajia kuanza siku ya Jumanne Januari 23, 2024 katika reli ya kati na kuelekea Mikoa ya Kaskazini (Tanga, Kilimanjaro na Arusha) inatarajiwa kuanza Januari 29, 2024 baada ya kukamilika uimarishaji wa miundombinu ya reli.

“TRC inaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza na inawasihi Wananchi kuwa wavumilivu katika kipindi cha matengenezo ili kuhakikisha usafiri unarejea katika hali ya usalama.”

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news