Tumuombee Rais Dkt.Samia akamilishe miradi ya maendeleo-Mbunge Dkt.Cherehani

NA SAMUEL MMBANGA

WATANZANIA wamehamasishwa kuendelea kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ili aweze kutekeleza na kukamilisha miradi ya maendeleo anayotekeleza.
Rai hiyo imetolewa Januari 7 na Mbunge wa Jimbo la Ushetu, Mhe. Dkt. Emmanuel Cherehani alipoongoza harambee kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa Kanisa la Mtakatifu Theresia, Parokia ya Chona Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.

Mhe. Cherehani amesema kuwa, Mhe. Rais Dkt. Samia amekuwa akitekeleza miradi mingi ya maendeleo nchini na katika Jimbo la Ushetu pia, huku akibainisha baadhi ya miradi hiyo ni kama ujenzi wa barabara, vituo vya afya, shule na madaraja ambapo miradi hiyo imelenga kuboresha maisha ya wananchi.
"Mhe. Rais Dkt. Samia anafanya kazi kubwa sana usiku na mchana kuhakikisha tunapata maendeleo. Sisi kama wananchi jukumu letu ni kumuunga mkono pamoja na kumuombea miradi hiyo ikamilike kwa ajili ya maendeleo yetu,"amesema Dkt.Cherehani.

Amesema kuwa, Rais Samia ametoa kiasi cha shilingi bilioni 4 kwa ajili ya ukarabati wa barabara na ujenzi wa madaraja katika Wilaya ya Ushetu.
Kadhalika, Dkt.Cherehani amesema kuwa,Rais Samia aametoa shilingi bilioni 1.8 kwa ajili ya vifaa vya kisasa katika zahanati na hospitali ya wilaya kwa ajili ya kuwahudumia wananchi bila kuwabagua.

Pia Dkt. Cherehani amesisitiza umuhimu wa wazazi na walezi kuhakikisha kuwa wanatenga muda wa kuzungumza na watoto wao ili kuimarisha malezi bora kwao na kulelewa katika maadili mema yanayompendeza Mungu.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa WAZOHURU MEDIA GROUP LIMITED ya jijini Dodoma, Mathias Canal amewasihi wananchi wa jimbo hilo kuendelea kumuombea na kumuunga mkono Mbunge wao, kwani wana kiongozi mwenye ari ya maendeleo, mpenda watu na mchapakazi.
Naye Bi.Neema Mgheni ambaye ni Mkurugenzi wa Gold Fm mjini Kahama amewasihi wananchi kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali jatika kuwaletea maendeleo huku akisisitiza umuhimu wa waumini kusikiliza na kufanyia kazi maelekezo ya viongozi wa dini katika kuimarisha maadili ya jamii.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news