Ujenzi wa barabara za juu Mwanakwerekwe na Amani utaondoa foleni Zanzibar-Rais Dkt.Mwinyi

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema ujenzi wa barabara za juu (Flyover) Mwanakwerekwe na Amani kuondoa tatizo la foleni Zanzibar.
Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo Januari 8,2024 alipoweka Jiwe la Msingi la ujenzi wa barabara ya kutoka uwanja wa ndege hadi Kiembe Samaki hadi Mnazi Mmoja, Mkoa wa Mjini Magharibi katika shamrashamra za Miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Aidha, Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa Serikali ya Awamu ya Nane imetekeleza kwa vitendo maagizo ya Ilani ya CCM na kuivuka.

Kwa upande mwingine Rais Dkt.Mwinyi amesema Serikali imejenga kilomita 200 za barabara ikiwemo ujenzi wa barabara za mjini kilomita 100 na vijijini kilomita 275.

Vile vile ujenzi wa barabara mpya zitazoanza hivi karibuni Tunguu hadi Makunduchi, Kisauni hadi Fumba, Chake hadi Mkoani zenye jumla ya kilomita 500.
Halikadhalika Rais Dkt.Mwinyi amewapongeza kampuni ya CECC ya China kwa ujenzi wa viwango vizuri vya barabara zikiwa na mitaro ya kupitisha maji, njia za watembea kwa miguu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news