VIDEO:Rais Dkt.Mwinyi ahimiza umuhimu wa mazoezi

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amewahimiza viongozi na wananchi kufanya mazoezi ili kulinda afya na kujikinga na maradhi yasiyoambukiza kutenga muda wa siku tatu kwa wiki angalau dakika thelathini.
Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo leo Januari 1,2024 katika Tamasha la Mazoezi ya Viungo kitaifa lililoshirikisha Vilabu 149 kutoka Unguja, Pemba na Tanzania Bara kwa matembezi yaliyoanzia Mnarani Kisonge mpaka Uwanja wa Amaan Mkoa wa Mjini Magharibi.
Kwa upande mwingine Rais Dkt.Mwinyi amehamasisha jamii kushiriki mazoezi na michezo kuepuka na vitendo viovu na magonjwa mbalimbali yasiyoambukiza.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news