KAMPALA-“Vitu lazima vitokee", ni msemo ambao ameutumia Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb) alipokutana na Mawaziri wenzake jijini Kampala, Uganda pembezoni mwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi Zisizofungamana na Upande Wowote (NAM) na Mkutano wa Kundi la Nchi 77+China tarehe 15 hadi 22 Januari 2024.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb) akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Algeria, Mhe. Ahmed Attaf. Mazungumzo hayo yalifanyika pembezoni mwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Mchi Zisizofungamana na Upande Wowote (NAM) uliofanyika Kampala, Uganda tarehe 15 hadi 20 Januari 2024.
Waziri Makamba ambaye alishiriki kwa siku tatu katika Mikutano hiyo alikutana na Mawaziri 17 kutoka nchi mbalimbali duniani kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia na nchi hizo na kuweka mikakati ya kushirikiana kiuchumi kwa manufaa ya pande zote.
Waziri Makamba aliifanya Mikutano hiyo ambayo imekusanya takriban theluthi mbili ya nchi zote duniani kama fursa muhimu ya kuitangaza Tanzania kidiplomasia na kujadili mikakati na nyenzo za kujiletea maendeleo na kutatua changamoto zinazoikabili dunia.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb) akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ghana, Mhe. Shirley Ayorkor Botchwey.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb) akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Msumbiji, Mhe. Veronica Macamo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb) akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Singapore, Mhe. . Dkt. Mohamad Maliki Bin Osman.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb) akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba, Mhe. Bruno Eduardo Rodriguez Parrilla.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb) akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Vietnam, Mhe. Do Hung Viet.
Mawaziri wa Mambo ya Nje waliokutana na Mhe. Makamba wanatoka nchi za Kenya, Msumbiji, Somalia, Malawi, Misri, Ghana, Morocco, Filipino, Ethiopia, Singapore, Vietnam, Cuba, Iraq, Bahamas, Venezuela, Jamhuri ya Kidemokrsia ya Congo na Azerbaijan.
Masuala muhimu ambayo Waziri Makamba ameyasisitiza kwa mawaziri wenzake ni kutumia nyezo za kawaida za kidiplomasia kukuza ushirikiano baina ya mataifa yao. Nyenzo hizo ni pamoja na Midahalo ya Kisiasa, Tume za Pamoja za Kudumu za Ushirikiano (JPCs), Mikutano ya Majukwaa ya Kiuchumi, Tume za Pamoja za Mawaziri (JMCs) na ziara za viongozi wa kitaifa.
Mhe. Makamba amesema kuwa endapo vyombo hivyo vitatumika ipasavyo vitatoa fursa kwa pande husika kukuza biashara, uwekezaji, utalii pamoja na kutatua changamoto zinazoweza kujitokeza katika utekelezaji wa masuala ambayo pande husika zimekubaliana.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb) akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri, Mhe. Sameh Shoukry.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb) akizungumza na Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje na Diaspora wa Jamhuri ya Kenya, Mhe. Dkt. Musalia Mudavadi.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb) akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Mhe. Christophe Lutundula.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb) akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Simalia, Mhe. Ali Mohammed Omar.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb) akizungumza na Waziri wa Uhamiaji na Bima ya Taifa wa Bahamas, Mhe. Alfred Sears.
Wakati wa mazungumzo na Mawaziri wa nchi za Singapore, Vietnam na Filipino, Mhe. Makamba alisema nchi hizo ni mfano wa kuigwa na nchi zinazoendelea duniani kutokana na kupiga hatua kubwa ya maendeleo kwa kipindi kifupi.
Alikubaliana na mawaziri wa nchi hizo kushirikiana katika mafunzo, hususan, kueendeleza rasilimali watu, utalii na kilimo.
Jambo lingine lililojitokeza ni ushirikiano katika ujenzi wa miundombinu na usafiri wa anga wa moja kwa moja baina ya mataifa. Waheshimiwa Mawaziri walijiridhisha bila shaka kuwa ukosefu wa miundombinu unakwamisha ufanyaji wa biashara na kuongeza gharama katika uzalishaji, hivyo wamesisitiza kutumia rasilimali za nchi zao kujiletea maendeleo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb) akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Aberzaijan, Mhe. Jeyhun Bayra.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb) akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia, Mhe. Mesganu Moach.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb) akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Morocco, Mhe. Nasser Bourita
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb) akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Philipino, Mhe. Enrique A. Manalo,
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb), akibadilishana mawasiliano na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iraq, Mhe. Omer Ahmed Berzinji.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb) akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Malawi, Mhe. Nancy Tembo.
Aidha, Mhe. Waziri alisisitiza umuhimu wa kutafuta suluhu kwa njia za kidiplomasia panapotokea migogoro ya kisiasa na aliwahakikishia viongozi wenzake kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na nchi nyingine katika utatuzi wa migogoro na ujenzi wa amani duniani.
Waziri Makamba katika kusimamia msemo wake wa “Vitu lazima vitokee" alikubaliana na viongozi wenzake kufufua makubaliano ya ushirikiano waliyojiwekea ili kuongeza kasi ya utekelezaji na kunzisha ushirikiano rasmi na nchi ambazo Tanzania haina mikataba rasmi ya ushirikiano.