Vyama vyakumbushwa kuzingatia ukomo wa muda wa viongozi, vyatakiwa kuzingatia matakwa ya sheria

DAR ES SALAAM-Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini imevikumbusha vyama ambavyo muda wa Uongozi wa Viongozi wake unakaribia kuisha, kufanya Uchaguzi wa Viongozi hao kabla ya muda huo haujaisha

Barua iliyotumwa kwa Makatibu Wakuu wa Vyama vya Siasa vyenye Usajili kamili leo, Alhamisi Januari 18,2024 imefafanua kuwa Kifungu cha 9(2)(e) kikisomwa pamoja na Kifungu cha 8D(1) cha Sheria 'The Political Parties Act, CAP 258' kinaelekeza kuwa, kila Chama cha Siasa kinapaswa kufanya Uchaguzi wa Kidemokrasia wa Viongozi wake kwa Vipindi ambavyo vimewekwa katika Katiba yake.

Aidha, Barua hiyo ambayo imesainiwa na Sisty Nyahoza ambaye ni Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa, kwa niaba ya Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini Jaji Francis Mutungi imeendelea kufafanua kuwa Kanuni ya 16 ya Kanuni 'The Political Parties (Registration and Monitoring) Regulations, 2019 (TS. 953/2019)' inaeleza kuwa Uchaguzi wa Viongozi wa Chama cha Siasa unapaswa kufanyika siyo zaidi ya miaka Mitano (5) tangu Uchaguzi uliopita kufanyika na kwamba Chama husika kitaomba ruhusa ya Msajili wa Vyama vya Siasa endapo kinataka kufanya Uchaguzi zaidi ya kipindi hicho;

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news