Waitwa kupima tezi dume kupitia PSA

DAR ES SALAAM-Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof. Mohamed Janabi amewataka kinababa kujitokeza kwa wingi kupima tezi dume kwa kutumia Njia Rahisi ya Damu (PSA).
Prof. Janabi ametoa rai hiyo Januari 27,2024 wakati akizumgumza na wananchi wa Ilala wakiongozwa na Mkuu wa wilaya hiyo, Mhe. Edward Mpogolo waliofika Hospitalini hapo kufanya usafi katika kumbukizi ya siku ya kuzaliwa ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

"Najua wengi mnaogopa kupima kwa sababu...ya ile njia nyingine...njooni tutatumia kipimo cha damu," amesisitiza Prof. Janabi.

Vile vile, Prof.Janabi ametaja dalili tano za tezi dume;

1. Maumivu wakati wa kupata haja ndoho.

2. Kuona damu katika haja ndogo au shahawa.

3. Kwenda haja ndogo mara kwa mara, lakini haja inatoka kidogo. Hasa mida ya usiku.

4. Kuhisi kuwa haja ndogo imebaki ndani ya kibofu baada ya kumaliza kujisaidia.

5. Nguvu dhaifu au ndogo ya kutoka haja ndogo.

6. Unapotaka kujisaidia haja ndogo, ukichelewa kufika msalani. Haja inaweza toka kidogo kwenye nguo yako ya ndani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news