NIAMEY-Nchi tatu za Afrika Magharibi zinazoongozwa na wanajeshi ikiwemo Jamhuri ya Niger, Mali na Burkina Faso zimesema zinajiondoa kwenye Jumuiya ya Uchumi ya Nchi za Afrika Magharibi ( ECOWAS).
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya pamoja iliyosomwa kwenye televisheni ya taifa ya Niger leo Januari 28,2024.
“Baada ya miaka 49, watu mashujaa wa Burkina Faso, Mali na Niger kwa masikitiko makubwa wanaona kwamba ECOWAS haizingatii tena maadili ya waasisi wake na msingi wa Afrika iliyoungana.
"Jumuiya hiyo ilishindwa kabisa kuzisaidia nchi hizo katika vita vyao dhidi ya ugaidi na usalama mdogo,” msemaji wa utawala wa kijeshi wa Niger, Kanali Abdramane Amadou amesema katika taarifa;