KATAVI-Wakulima 72 wa Mkoa wa Katavi wamenufaika na mafunzo ya matumizi sahihi ya mbolea.
Afisa Udhibiti Ubora wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA),Chimile Mfugale akitoa elimu ya matumizi sahihi ya mbolea kwa wakulima Wilaya ya Tanganyika katika shamba darasa ambalo wakulima wameelimishwa matumizi sahihi ya mbolea, matumizi ya mbegu bora, palizi na udhibiti wa visumbufu vya mimea yaliyotolewa kwa kushirikiana na kampuni ya Seedco.
Ni baada ya wataalam kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Kanda ya Nyanda za Juu Kusini na wadau wake kutoka kampuni ya mbolea ya OCP Tanzania Ltd na wazalishaji wa mbegu wa Seedco kutoa mafunzo hayo kwa wakulima.
Mafunzo na uhamasishaji huo wa matumizi sahihi ya mbolea umefanyika Januari 17, 2024 katika Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda katika Kata ya Magamba na Kakese ambapo jumla ya wakulima 46 wamehamasishwa juu ya matumizi sahihi ya mbolea.
Awali, wakulima 26 wa Kata ya Katuma katika Kijiji cha Kapanga Halmashauri ya Wilaya Tanganyika walifikiwa na elimu hiyo na kufanya jumla ya wakulima 72 waliofikiwa na elimu ya matumizi sahihi ya mbolea katika wilaya hiyo.
Akizungumza kwa niaba ya wanufaika wa mafunzo hayo, Mkulima PIASON KALWIHO MTAFYA wa Kijiji cha Kapanga kati Kata ya Katuma Wilaya ya Tanganyika, mkoani Katavi, ameishukuru Serikali kwa Kuja na mpango wa ruzuku na kueleza mpango huo umeleta nafuu kubwa kwa wakulima kwa awali walikuwa wakununua mbolea kwa bei kubwa ya shilingi 150,000 ambapo wakulima wengi hawakumudu na hivyo kuzalisha kidogo.
Afisa Udhibiti Ubora wa TFRA, Henerico Renatus akitoa elimu ya matumizi sahihi ya mbolea kwa wakulima wa kijiji cha Nakayaya Wilayani Tunduru. Hapo ni katika shamba ambalo lilipandwa mahindi bila kuwekwa mbolea na mimea imeonesha dhahili upungufu wa virutubisho vya Nitrogen na Phosphorus hivyo mkulima hata pata tija ya uzalishaji kama inavyotakiwa kwa eneo. Elimu hiyo inatolewa na timu ya wataalam wa kampuni ya Seedco, TFRA na kampuni ya mbolea ya OCP Tanzania Limited.
Ameishukuru TFRA na washirika wake kwa kuja na mpango wa kuwaelimisha kupitia mashamba darasa na kueleza imesaidia kuondoa mtazamo hasi waliokuwa nao kuwa, mbolea inaharibu udongo.
Sambamba na mafunzo hayo, Kanda hiyo inaendelea na mafunzo katika mikoa ya Njombe, Songea na wilaya za Ludewa Tunduru kata ya Nakayaya wakiwa na lengo la kuwafikia wakulima 500 Katika Mikoa 7 Halmashauri 40 za Nyanda za Juu Kusini.