GEITA-Changamoto ya upungufu wa viti na meza za walimu katika Shule ya Msingi Nyansalala iliyoko Kata ha Bukondo Halmashauri ya Wilaya ya Geita mkoani Geita imepatiwa ufumbuzi.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) ambapo shule hiyo ina jumla ya walimu 12 wa kike sita na wa kiume sita.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, katika Ofisi ya Walimu kulikua na upungufu wa viti na meza za walimu ambapo hivi karibuni walionekana walimu hao kukalia madaftati wanapofanya kazi zao.
"Kamati ya shule kwa kutambua changamoto ya uhaba wa meza na viti kwa ajili ya walimu, ilikaa na kufikia maamuzi ya kutengeneza viti nane na meza nane kupitia Ruzuku ya Serikali ya Uendeshaji wa Shule (Capitation Grants) ili walimu waweze kupata meza na viti kwa ajili ya kazi zao.
"Viti nane na meza nane tayari vipo tayari shuleni kwa kwa ajili ya matumizi.Tunatoa pole kwa walimu wetu kwa usumbufu uliojitokeza na kazi iendelee,"imefafanua sehemu ya taarifa hiyo.