NA DIRAMAKINI
BARAZA la Mitihani la Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha nne uliofanyika Novemba 13 hadi 30, 2023.Matokeo ya Kidato cha Nne 2023 haya hapa》》》
Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Dkt. Said Mohamed ametangaza matokeo hayo Januari 25,2024 jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa, jumla ya watahiniwa 484,823 sawa na asilimia 87.65 ya watahiniwa waliofanya Mtihani wa Kidato cha Nne 2023 wamefaulu.Matokeo ya Kidato cha Nne 2023 haya hapa》》》
“Mwaka 2022 watahiniwa waliofaulu walikuwa 476,450 sawa na asilimia 86.78, hivyo ufaulu umeongezeka kwa asilimia 0.87 ikilinganishwa na mwaka 2022,” amesema Dkt.Mohamed.
Aidha,kwa mwaka 2023 watahiniwa 572,359 walisajiliwa kufanya mtihani huo wa kidato cha nne ambapo watahiniwa wa shule walikuwa 543,332 na watahiniwa wa kujitegemea walikuwa 29,027.Matokeo ya Kidato cha Nne 2023 haya hapa》》》
Kati ya watahiniwa hao wasichana walikuwa 310,248 sawa na asilimia 54.21 na wavulana walikuwa 262,111.
Mwaka 2022 watahiniwa waliopata ufaulu wa daraja la kwanza hadi la tatu walikuwa 192,348 sawa na asilimia 36.95, kulinganisha na watahiniwa 197,426 waliopata madaraja hayo mwaka 2023.Matokeo ya Kidato cha Nne 2023 haya hapa》》》