Waziri Aweso:Tunachukua hatua, mtu wa manunuzi Lindi asimame kazi

SHINYANGA-Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amemuelekeza Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Prof.Jamali Katundu kuhakikisha hatua stahiki za kiofisi zinachukuliwa kwa wahusika wote mkoani Lindi waliosababisha uzembe katika kazi iliyotakiwa kufanywa na mitambo ya uchimbaji.
Sambamba na ununuzi wa pikipiki ambazo zimeachwa stoo kwa muda mrefu katika stoo ya Wakala ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mkoa wa Lindi.

Katika hatua nyingine amemtaka Katibu Mkuu kwa taratibu za kiutumishi kumsimamisha mtu Manunuzi wa Mamlaka ya Maji na usafi wa Mazingira Lindi,Kennedy Mbagwa kwa hatua zaidi.

Kutotumika kwa vitendea kazi hivyo kumebainika wakati wa ziara ya Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) katika ofisi za RUWASA mkoani Lindi.
Waziri Aweso amesema, hatua za kiofisi zinachukuliwa mara moja na Wizara ya Maji.

Amesema hayo wakati akikagua hali ya uzalishaji maji katika mtambo wa Ihelele unaosimamiwa na Mamlaka ya Maji ya Kahama (KASHWASA) mkoani Shinyanga.

Mhe. Aweso amewataka watendaji katika Sekta ya Maji kila mmoja atimize wajibu wake katika kuwahudumia wananchi na kwamba hatosita kuchukua hatua pale uzembe utakapobainika.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news