DAR ES SALAAM-Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu amekutana na wawakilishi wa wamiliki wa vituo vya afya nchini ambao ni watoa huduma za Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa lengo la kujadili Kitita cha Mafao kwa wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.

Katika kikao hicho, Waziri Ummy amewataka wawakikishi hao kujadiliana na kutoa maoni yao kwa uwazi na kwa kutanguliza maslahi mapana ya Watanzania ili kuwezesha upatikanaji wa huduma za matibabu kwa wananchi bila kikwazo cha fedha.
Kikao hicho kimehudhuriwa na Katibu Mkuu Wizara ya1 Afya Dkt. John Jingu, Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu, Mwenyekiti wa APHFTA Dkt. Egina Makwabe, Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF,Bw. Juma Muhimbi, Mfamasia Mkuu wa Serikali, Bw. Daud Msasi na Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bw. Bernard Konga.
Pia, wawakilishi kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) pamoja na wawakilishi kutoka Bohari ya Dawa (MSD).