DAR ES SALAAM-Balozi mstaafu wa Tanzania nchini Ubelgiji, na Waziri wa zamani wa Afrika Mashariki Dkt.Diodorus Kamala amefariki dunia leo jijini Dar es Salaam akiwa na umri wa miaka 55.
Dkt. Deodorus Buberwa Kamala amefariki dunia akiwa anapatiwa matibabu Hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam.
Wakati wa uhai wake amewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Nkenge Wilaya ya Missenyi Mkoa wa Kagera kuanzia mwaka 2000 hadi 2010.
Aidha, mwaka 2006 aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Afrika Mashariki na baadaye Waziri kamili mwaka 2008 hadi 2010.
Mwaka 2011 aliteuliwa kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Ubelgiji na Uholanzi ambako alitumikia nafasi hiyo hadi mwaka 2015 aliporejea kuwa Mbunge hadi mwaka 2020.
Uzoefu katika siasa
Political Party | Position | From | To |
---|---|---|---|
Chama Cha Mapinduzi | National Youth Secretary-UVCCM | 2000 | 2002 |
Foreign Affairs and Defence Committee of the Parliament | Member | 2005 | 2010 |
Chama Cha Mapinduzi | Secretary of promotions and Sprout UVCCM | 2002 | 2007 |
Chama Cha Mapinduzi | Member-Ntional Executive Council | 2002 | 2007 |
Economics and Finance Committee of the Parliament | Member | 2000 | 2002 |
IDM-Mzumbe | President of the Student Union | 1994 | 1995 |
Local Authorities Accounts Committee of the Government | Member | 2003 | 2005 |
Parliament of Tanzania | Member of the Parliament | 2005 | 2010 |
Parliament of Tanzania | Member of the Parliament | 2015 | 2020 |
Parliament of Tanzania | Member of the Parliament | 2000 | 2005 |
Industries, Trade and Enviroment Committee | Member | 2015 | 2018 |