DAR ES SALAAM-Balozi wa Urusi nchini Tanzania, Mhe. Andrey Avetsyan ametembelea ofisi za Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) jijini Dar es Salaam leo Februari 21, 2024.
Lengo la ziara hii ni kujitambulisha kwa Kamishna Jenerali Aretas Lyimo na kujadili namna ya kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Urusi katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya.
Pamoja na mambo mengine, Balozi Avetsyan amempongeza Kamishna Jenerali Lyimo kwa ukamataji mkubwa wa kilo 3,522.52 wa dawa za kulevya uliofanyika Desemba,2023.