DAR ES SALAAM-Benki Kuu ya Tanzania (BoT) tarehe 15 Februari 2024 imeendesha kikao elimishi kwa mabenki na taasisi nyingine za fedha kuhusu miongozo ya kiutendaji ya Mfuko wa Udhamini wa Mikopo kwa ajili ya Mauzo Nje ya Nchi (ECGS) na Mfuko wa Udhamini wa Mikopo kwa Wajasiriamali Wadogo na wa Kati (SMEs-CGS).
Akifungua kikao hicho, Kaimu Mkurugenzi wa Ustawi na Huduma Jumuishi za Fedha, Bi. Nangi Massawe, alisema mifuko hiyo ilianzishwa na serikali kwa lengo la kuimarisha miundombinu itakayosaidia miradi ya mbalimbali ya biashara inayokosa dhamana kupata mikopo kutoka kwa mabenki na taasisi nyingine za fedha.
Bi. Massawe alizihimiza taasisi hizo kuwa na tathmini na usimamizi mzuri wa waombaji udhamini ili kupunguza mikopo chechefu.



Serikali ilianzisha mifuko ya ECGS) mwaka 2002 na SMEs-CGS mwaka 2005.
Tags
Benki za Tanzania
Benki Kuu ya Tanzania
Habari
Sekta ya Fedha Tanzania
Sekta ya Mabenki Tanzania
Taasisi za Kifedha Tanzania