Bunge lapitisha miswada mitatu ya uchaguzi

DODOMA-Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha muswada wa sheria ya Tume ya Taifa ya uchaguzi, muswada wa sheria ya uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani na muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria ya vyama vya siasa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama akitoa ufafanuzi kuhusu hoja za wabunge zilizowasilishwa wakati wa majadiliano ya miswada ya sheria ya uchaguzi katika Bunge linaloendelea Jijini Dodoma tarehe 02, 2024.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderianana akichangia maoni yake kuhusu miswada ya sheria ya uchaguzi wakati wa Bunge linaloendelea Jijini Dodoma tarehe 02 Februari, 2024.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akitambulishwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson wakati alipohudhuria Bunge la 12 Mkutano wa 14 kikao cha Nne tarehe 02, Februari 2024 Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi (kulia) akiteta jambo na Naibu wake Bw. Anderson Mutatembwa wakati wa Bunge linaloendelea jijini Dodoma tarehe 02 Februari, 2024.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama akiteta jambo na Katibu Mkuu wa Ofisi yake Dkt. Jim Yonazi mara baada ya kupitishwa kwa miswada ya sheria ya Uchaguzi katika Bunge linaloendelea jijini Dodoma tarehe 02, Februari 2024.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderianana akizungumza na Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Dkt. Jim Yonazi mara baada ya kupitishwa kwa miswada ya sheria ya Uchaguzi katika Bunge linaloendelea Jijini Dodoma tarehe 02, Februari 2024.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama (wa tatu kulia) na Naibu Wake Mhe. Ummy Nderiananga wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa fisi yake mara baada ya kupitishwa kwa miswada ya sheria ya Uchaguzi katika Bunge linaloendelea Jijini Dodoma tarehe 02, Februari 2024.(Picha na OWM).

Miswada hiyo mitatu imepitishwa mara baada ya kujadiliwa na wabunge katika mkutano wa 14 wa Bunge linaloendelea Jijini Dodoma Februari 02, 2024 ambapo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama alitoa ufafanuzi kuhusu hoja za wabunge zilizowasilishwa wakati wa majadiliano ya miswada ya sheria ya uchaguzi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news