Changamkieni fursa za Sekta ya Utalii-Rais Dkt.Mwinyi

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amewataka wananchi kuchangamkia fursa mbalimbali za sekta ya utalii ikiwemo ajira, kuuza mazao wanayozalishwa nchini na usafirishaji.
Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo leo Februari 21,2024 alipofungua Mkutano wa Pili wa Kimataifa wa sekta ya utalii na Maonesho "The Z Summit 2024" katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip, Uwanja wa Ndege Zanzibar.

Aidha,Rais Dkt.Mwinyi amesema, Serikali itaendelea kujenga miundombinu ya ujenzi wa barabara mpya, kuboresha usambazaji wa umeme na maji pamoja na viwanja vya ndege.

Halikadhalika, Rais Dkt.Mwinyi amesema Sheria mpya ya uwekezaji Zanzibar ya mwaka 2024 imeweka vivutio vingi ambavyo vinalinda uwekezaji na kuwa vivutio vya kodi Afrika Mashariki.

Kwa upande mwingine Rais Dkt.Mwinyi amesema Pemba ni chachu ya ukuaji wa uchumi na maendeleo ya baadae kwa kuanzishwa Ukanda wa Uwekezaji wa Pemba (PIZ) ili kuvutia wawekezaji na kuchochea shughuli za kiuchumi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news