DAR ES SALAAM-Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini zitakazotumika kuanzia Jumatano, tarehe 7 Februari 2024 saa 6:01 usiku.
EWURA imefafanua kuwa,kupungua kwa bei za mafuta kwa mwezi Februari 2024 kunatokana na kushuka kwa bei za mafuta (FOB) katika soko la dunia kwa wastani (weighted average) wa asilimia 10.66 kwa petroli, asilimia 11.20 kwa dizeli na asilimia 5.82 kwa mafuta ya taa.
Pia kupungua kwa bei za mafuta kumetokana na kushuka kwa gharama za uagizaji wa mafuta kwa Bandari ya Dar es Salaam kwa wastani (weighted average) wa asilimia 9.69 kwa dizeli na asilimia 1.82 kwa mafuta ya taa.
Vivyo hivyo, gharama za uagizaji wa mafuta ya petroli na dizeli kwa Bandari za Tanga na Mtwara zimepungua kwa wastani (weighted average) wa asilimia 0.69 na 11.93, mtawalia.
Wafanyabiashara wa bidhaa za mafuta kwa rejareja wanatakiwa kuuza mafuta kwa bei zinazooneshwa katika Jedwali Na. 3. Aidha, wafanyabiashara wa bidhaa za mafuta kwa jumla wanatakiwa kuuza mafuta kwa bei zinazooneshwa katika Jedwali Na. 2.
Hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mfanyabiashara yoyote atakayekiuka agizo hili;