Fanikisha Limited yafungiwa kwa kutoa huduma kinyume na sheria,mikopo ya kausha damu

ZANZIBAR-Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Fedha na Mipango, Dkt. Saada Mkuya Salum ameifungia Kampuni ya Fanikisha Limited kutoa huduma kunzia Februari 21, 2024 kutokana na kutoa huduma kinyume na sheria.
Ameyasema hayo wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika Kampuni ya Fanikisha Limited inayojishughulisha na Utoaji wa Huduma za Fedha huko Mpendae Wilaya ya Mjini.

Amesema,kampuni hiyo inatoa huduma bila kibali kutoka Wizara ya Nchi,Ofisi ya Rais Fedha na Mipango jambo ambalo ni kinyume na miongozo na taratibu na sheria iliyowekwa na Serikali.

Aidha, amesema Kampuni ya Fanikisha Limited inatoza kiwango cha riba ya mikopo cha asilimia 15 kwa mwezi badala ya kiwango cha asilimia 3.5 kilichowekwa na ofisi.
Hata hivyo, mikopo iliyokuwa inatolewa na Kampuni ya Fanikisha Limited ni mikopo ya kausha damu.

Katika ziara hiyo,Mhe. Dkt. Saada ameongozana na Kamishna wa Sera za Kodi na Fedha wa Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar,Haji A. Haji.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news