Gavana Tutuba ateta na viongozi wa NMB, BOA

DAR ES SALAAM-Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Emmanuel Tutuba, amekutana na kufanya mazungumzo na benki za NMB na Bank of Africa (BOA) katika ofisi za makao makuu ndogo ya Benki Kuu jijini Dar es Salaam.
Katika vikao hivyo vilivyofanyika kwa nyakati tofauti Februari 2, 2024, Gavana na viongozi kutoka NMB na BOA wamejadiliana mambo mbalimbali kuhusu ukuaji wa sekta ya fedha na uchumi nchini.

Aidha, taasisi hizo zimeeleza mikakati mbalimbali waliyonayo katika kukuza sekta ya fedha na huduma jumuishi za fedha.

Gavana Tutuba amezipongeza taasisi hizo kwa juhudi mbalimbali wanazofanya na kuwaasa kuendelea kuisadia jamii, kusimamia vyema utekelezaji wa mikakati waliyonayo na kuzingatia taratibu zinazowaongoza pamoja na miongozo inayotolewa na Benki Kuu ya Tanzania.
Pia, ameahidi kuwa Benki Kuu itaendelea kutoa ushirikiano kwa taasisi zote za fedha nchini ili kuchochea maendeleo endelevu kwenye sekta ya fedha.

Ujumbe wa Benki ya NMB uliongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Bi. Ruth Zaipuna na Ujumbe wa Benki ya BOA uliongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki za BOA, Bw. Amine Bouabid.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news